21. Nendeni, mkamwulize Bwana kwa ajili yangu, na kwa hao waliosalia wa Israeli na wa Yuda, katika habari za maneno ya kitabu kilichoonekana; maana ghadhabu ya Bwana ni nyingi iliyomwagika juu yetu, kwa sababu baba zetu hawakulishika neno la Bwana, kutenda sawasawa na yote yaliyoandikwa kitabuni humo.