Bible Study: FrontPage




 

1 Wakorintho, Chapter 13

Bible Study - 1 Wakorintho 13 - Swahili - Swahili New Testament - Web
 
 
 
Comment!       Comment Disqus!
  
1. Hata kama nikinena lugha za watu na hata za malaika, lakini kama sina upendo mimi nimekuwa tu kama sauti ya debe tupu au kengele.
  
2. Tena, naweza kuwa na kipaji cha kutangaza ujumbe wa Mungu, nikafahamu siri zote na kujua kila kitu; naweza kuwa na imani yote hata nikawezakuihamisha milima, lakini kama sina upendo mimi si kitu.
  
3. Nikitoa mali yangu yote na kuwapa maskini, na tena nikiutoa mwili wangu uchomwe, kama sina upendo hiyo hainifai chochote.
  
4. Mwenye upendo huvumilia, hufadhili; mwenye upendo hana wivu, hajidai, wala hajivuni.
  
5. Mwenye upendo hakosi adabu, hatafuti faida yake binafsi, wala hana wepesi wa hasira; haweki kumbukumbu ya mabaya,
  
6. hafurahii uovu, bali hufurahia ukweli.
  
7. Mwenye upendo huvumilia yote, huamini yote, na hustahimili yote.
  
8. Upendo hauna kikomo kamwe. Kama kuna vipaji vya kutangaza ujumbe wa Mungu, hivyo vitatoweka siku moja; kama ni vipaji vya kusema lughangeni, vitakoma; kama kuna elimu, nayo itapita.
  
9. Maana ujuzi wetu si kamili, na kipaji chetu cha kutangaza neno la Mungu si kamili.
  
10. Lakini kile kilicho kikamilifu kitakapofika, vyote visivyo vikamilifu vitatoweka.
  
11. Nilipokuwa mtoto mchanga nilisema kitoto, nilifahamu kitoto, nilifikiri kitoto. Lakini sasa, maadam mimi ni mtu mzima, mambo yakitoto nimeyaacha.
  
12. Tunachoona sasa ni kama tu sura hafifu katika kioo, lakini hapo baadaye tutaona uso kwa uso. Sasa ninajua kiasi fulani tu, lakini hapobaadaye nitajua yote kikamilifu, kama vile Mungu anavyonijua mimi.
  
13. Sasa yanadumu haya matatu: imani, tumaini na upendo; lakini lililo kuu kupita yote ni upendo.


Search in:
Terms:

Vote and Comment on Facebook:Recommend This Page:
Post on Facebook Add to your del.icio.us Digg this story StumbleUpon Twitter Google Plus Post on Tumblr Add to Reddit Pin this story Linkedin Google Bookmark Blogger
Insert Your Personal Insight:

Please do not make mean comments and follow the biblical and spiritual character of this forum. If, however unpleasant situations arise, we request to flag it to us in order to evaluate the situation.

Text source: Swahili New Testament, public domain.

This project is based on delivering free-of-charge the Word of the Lord in all the world by using electronic means. If you want to contact us, you can do this by writing to the following e-mail: bible-study.xyz@hotmail.com


SELECT VERSION

COMPARE WITH OTHER BIBLES