Bible Study: FrontPage




 

1 Timotheo, Chapter 5

Bible Study - 1 Timotheo 5 - Swahili - Swahili New Testament - Web
 
 
 
Comment!       Comment Disqus!
  
1. Usimkemee mtu mzee, bali msihi kama vile angekuwa baba yako. Watendee vijana kama ndugu zako,
  
2. wanawake wazee kama mama yako, na wasichana kama dada zako, kwa usafi wote.
  
3. Waheshimu wanawake wajane walio wajane kweli.
  
4. Lakini mjane aliye na watoto au wajukuu, hao wanapaswa kujifunza kutimiza wajibu wao wa kidini kwa jamaa zao wenyewe na hivyo kuwalipawazazi wao na wazee wao, kwani hilo ni jambo la kupendeza mbele yaMungu.
  
5. Mwanamke mjane kweli, asiye na mtu wa kumsaidia, amemwekea Mungu tumaini lake na huendelea kusali na kumwomba msaada usiku na mchana.
  
6. Lakini mwanamke ambaye huishi maisha ya anasa, huyo amekufa, ingawa yu hai.
  
7. Wape maagizo haya, wasije wakawa na lawama.
  
8. Lakini kama mtu hawatunzi watu wa jamaa yake, hasa wale wa nyumbani kwake, basi, mtu huyo ameikana imani, na ni mbaya zaidi kuliko mtuasiyeamini.
  
9. Usimtie katika orodha ya wajane, mjane yeyote ambaye hajatimiza miaka sitini. Tena awe amepata kuolewa mara moja tu,
  
10. na awe mwenye sifa nzuri: aliyewalea watoto wake vizuri, aliyewakaribisha wageni nyumbani kwake, aliyewaosha miguu watu waMungu, aliyewasaidia watu wenye taabu, na aliyejitolea kufanya mambomema.
  
11. Usiwaandikishe wajane vijana, kwani kama tamaa zao za maumbile zikizidi kuwa na nguvu zaidi kuliko kujitolea kwao kwa Kristo watatakakuolewa tena,
  
12. na wataonekana kukosa uaminifu kuhusu ahadi yao ya pale awali.
  
13. Wajane kama hao huanza kupoteza wakati wao wakizurura nyumba hata nyumba; tena ubaya zaidi ni kwamba huanza kuwasengenya watu, nakujitia katika mambo ya watu wengine, huku wakisema mambo ambayohawangepaswa kusema.
  
14. Kwa hiyo ningependelea wajane vijana waolewe, wapate watoto na kutunza nyumba zao ili adui zetu wasipewe nafasi ya kusema mambo maovujuu yetu.
  
15. Kwa maana wajane wengine wamekwisha potoka na kumfuata Shetani.
  
16. Lakini kama mama Mkristo anao wajane katika jamaa yake, yeye anapaswa kuwatunza na si kuliachilia kanisa mzigo huo, ili kanisaliweze kuwatunza wajane wale waliobaki peke yao kabisa.
  
17. Wazee wanaowaongoza watu vizuri wanastahili kupata riziki maradufu, hasa wale wanaofanya bidii katika kuhubiri na kufundisha.
  
18. Maana Maandiko Matakatifu yasema: "Usimfunge ng`ombe kinywa anapopura nafaka." na tena "Mfanyakazi astahili malipo yake."
  
19. Usikubali kupokea mashtaka dhidi ya mzee yasipowakilishwa na mashahidi wawili au watatu.
  
20. Wale wanaotenda dhambi waonye hadharani, ili wengine wapate kuogopa.
  
21. Nakuamuru mbele ya Mungu, mbele ya Kristo Yesu, na mbele ya malaika watakatifu uyazingatie maagizo haya bila kuacha hata moja, walakumpendelea mtu yeyote katika kila unachotenda.
  
22. Usiharakishe kumwekea mtu yeyote mikono kwa ajili ya kumtumikia Bwana. Usishiriki dhambi za wengine; jiweke katika hali safi.
  
23. Usinywe maji tu, bali unywe divai kidogo kwa ajili ya tumbo lako, kwani unaugua mara kwa mara.
  
24. Dhambi za watu wengine huonekana waziwazi, nazo zawatangulia kwenye hukumu; lakini dhambi za wengine huonekana tu baadaye.
  
25. Vivyo hivyo, matendo mema huonekana waziwazi, na hata yale ambayo si dhahiri hayawezi kufichika.


Search in:
Terms:

Vote and Comment on Facebook:Recommend This Page:
Post on Facebook Add to your del.icio.us Digg this story StumbleUpon Twitter Google Plus Post on Tumblr Add to Reddit Pin this story Linkedin Google Bookmark Blogger
Insert Your Personal Insight:

Please do not make mean comments and follow the biblical and spiritual character of this forum. If, however unpleasant situations arise, we request to flag it to us in order to evaluate the situation.

Text source: Swahili New Testament, public domain.

This project is based on delivering free-of-charge the Word of the Lord in all the world by using electronic means. If you want to contact us, you can do this by writing to the following e-mail: bible-study.xyz@hotmail.com


SELECT VERSION

COMPARE WITH OTHER BIBLES