Bible Study: FrontPage




 

Marko, Chapter 12

Bible Study - Marko 12 - Swahili - Swahili New Testament - Web
 
 
 
Comment!       Comment Disqus!
  
1. Yesu alianza kusema nao kwa mifano: "Mtu mmoja alilima shamba la mizabibu. Akalizungushia ukuta, na katikati yake akachimba kisima chakusindikia divai, akajenga mnara pia. Akalikodisha shamba hilo kwawakulima, akasafiri hadi nchi ya mbali.
  
2. Wakati wa mavuno, alimtuma mtumishi wake kwa wale wakulima akamletee sehemu ya mazao ya shamba lake.
  
3. Wale wakulima wakamkamata, wakampiga, wakamrudisha mikono mitupu.
  
4. Akatuma tena mtumishi mwingine; huyu wakamuumiza kichwa na kumtendea vibaya.
  
5. Mwenye shamba akatuma mtumishi mwingine tena, na huyo wakamuua. Wengine wengi waliotumwa, baadhi yao walipigwa, na wengi wakauawa.
  
6. Alibakiwa bado na mtu mmoja, yaani mwanawe mpendwa. Mwishowe akamtuma huyo akisema, `Watamheshimu mwanangu.`
  
7. Lakini hao wakulima wakaambiana, `Huyu ndiye mrithi, basi, tumuue ili urithi wake uwe wetu!`
  
8. Kwa hiyo wakamkamata, wakamuua na kumtupa nje ya lile shamba la mizabibu. ic Mnara ndani ya shamba la mizabibu (Marko 12:1)
  
9. "Basi, mwenye shamba atafanya nini? Atakuja kuwaangamiza hao wakulima na kulikodisha hilo shamba la mizabibu kwa watu wengine.
  
10. Je, hamjasoma Maandiko haya? `Jiwe walilokataa waashi sasa limekuwa jiwe kuu la msingi.
  
11. Bwana ndiye aliyefanya jambo hili, nalo ni la ajabu sana kwetu."`
  
12. Makuhani wakuu, walimu wa Sheria na wazee walifahamu ya kwamba mfano huo ulikuwa unawahusu. Kwa hiyo walijaribu kumtia nguvuni, lakiniwaliogopa umati wa watu. Basi, wakamwacha wakaenda zao.
  
13. Basi, baadhi ya Mafarisayo na wafuasi wa kikundi cha Herode walitumwa ili wamtege Yesu kwa maneno yake.
  
14. Wakamwendea, wakamwambia, "Mwalimu, tunajua kwamba wewe ni mtu mwaminifu unayesema ukweli mtupu, wala humjali mtu yeyote. Wala cheocha mtu si kitu kwako, lakini wafundisha ukweli kuhusu njia ya Mungu.Je, ni halali kulipa kodi kwa Kaisari, au la? Tulipe au tusilipe?"
  
15. Lakini Yesu alijua unafiki wao, akawaambia, "Mbona mnanijaribu? Nionyesheni sarafu."
  
16. Wakamwonyesha. Naye akawauliza, "Sura na chapa hii ni ya nani?" Wakamjibu, "Ni ya Kaisari."
  
17. Basi, Yesu akawaambia, "Mpeni Kaisari yaliyo yake Kaisari na Mungu yaliyo yake Mungu." Wakashangazwa sana naye.
  
18. Masadukayo wasemao kwamba hakuna ufufuo walimwendea Yesu, wakamwuliza,
  
19. "Mwalimu, Mose alituagiza hivi: `Mtu akifa na kuacha mke bila mtoto, ndugu yake lazima amchukue huyo mama mjane amzalie watoto ndugu yakemarehemu.`
  
20. Basi, kulikuwa na ndugu saba. Wa kwanza alioa, akafa bila kuacha mtoto.
  
21. Ndugu wa pili akamwoa huyo mjane, naye pia akafa bila kuacha mtoto; na ndugu watatu hali kadhalika.
  
22. Wote saba walikufa bila kuacha mtoto. Mwishowe yule mama mjane naye akafa.
  
23. Basi, siku watu watakapofufuka, mama huyo atakuwa mke wa nani? Maana wote saba walikuwa wamemwoa."
  
24. Yesu akawaambia, "Ninyi mmekosea sana, kwa sababu hamjui Maandiko Matakatifu wala nguvu ya Mungu.
  
25. Maana wafu watakapofufuka, hawataoa wala kuolewa; watakuwa kama malaika wa mbinguni.
  
26. Lakini kuhusu kufufuliwa kwa wafu, je, hamjasoma kitabu cha Mose katika sehemu inayohusu kile kichaka kilichokuwa kinawaka moto? Mungualimwambia Mose, `Mimi ni Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaka, na Munguwa Yakobo.`
  
27. Basi, yeye si Mungu wa wafu, bali ni Mungu wa walio hai. Ninyi mmekosea sana!"
  
28. Mmojawapo wa walimu wa Sheria alifika, akasikia mabishano yao. Alipoona kwamba Yesu aliwajibu vyema, akajitokeza akamwuliza, "Katikaamri zote ni ipi iliyo ya kwanza?"
  
29. Yesu akamjibu, "Ya kwanza ndiyo hii: `Sikiliza, Israeli! Bwana Mungu wetu ndiye peke yake Bwana.
  
30. Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, kwa akili yako yote na kwa nguvu zako zote.`
  
31. Na ya pili ndiyo hii: `Mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe.` Hakuna amri nyingine iliyo kuu kuliko hizi."
  
32. Basi, yule mwalimu wa Sheria akamwambia, "Vyema Mwalimu! Umesema kweli kwamba Mungu ni mmoja tu wala hakuna mwingine ila yeye.
  
33. Na ni lazima mtu kumpenda Mungu kwa moyo wote, kwa akili yote, na kwa nguvu zote, na kumpenda jirani yake kama anavyojipenda mwenyewe.Jambo hili ni muhimu zaidi kuliko dhabihu na sadaka zote zakuteketezwa."
  
34. Yesu alipoona kwamba huyu mtu alimjibu kwa ujasiri, akamwambia, "Wewe huko mbali na Ufalme wa Mungu." Baada ya hayo, hakuna mtualiyethubutu tena kumwuliza kitu.
  
35. Wakati Yesu alipokuwa akifundisha Hekaluni, aliuliza, "Mbona walimu wa Sheria wanasema ya kwamba Kristo ni mwana wa Daudi?
  
36. Daudi mwenyewe akiongozwa na Roho Mtakatifu alisema: `Bwana alimwambia Bwana wangu: Keti upande wangu wa kulia, Mpakanitakapowaweka adui zako chini ya miguu yako."`
  
37. "Daudi mwenyewe anamwita Kristo Bwana. Basi, Kristo atakuwaje mwanae?" Umati wa watu ulikuwa ukimsikiliza kwa furaha.
  
38. Katika mafundisho yake, Yesu alisema, "Jihadharini na walimu wa Sheria ambao hupenda kupitapita wamejivalia kanzu ndefu na kusalimiwana watu kwa heshima sokoni; hupenda kuketi mahali pa heshima katikamasunagogi,
  
39. na kuchukua nafasi za heshima katika karamu.
  
40. Huwanyonya wajane huku wakijisingizia kusali sala ndefu. Siku ya hukumu watapata adhabu kali!"
  
41. Yesu alikuwa ameketi karibu na sanduku la hazina. Akawa anatazama jinsi watu wengi walivyokuwa wakitoa fedha na kuzitia katika hazina yaHekalu. Matajiri wengi walitoa fedha nyingi.
  
42. Hapo akaja mama mmoja mjane maskini, akatoa sarafu mbili ndogo za fedha.
  
43. Yesu akawaita wanafunzi wake, akawaambia, "Kweli nawaambieni, huyu mama mjane maskini ametoa zaidi kuliko wengine wote waliotia fedhakatika sanduku la hazina.
  
44. Maana wote walitoa kutokana na ziada ya mali zao, lakini huyu mama, ingawa ni maskini, ametoa yote aliyokuwa nayo, ametoa kila kitualichohitaji kwa kuishi."


Search in:
Terms:

Vote and Comment on Facebook:Recommend This Page:
Post on Facebook Add to your del.icio.us Digg this story StumbleUpon Twitter Google Plus Post on Tumblr Add to Reddit Pin this story Linkedin Google Bookmark Blogger
Insert Your Personal Insight:

Please do not make mean comments and follow the biblical and spiritual character of this forum. If, however unpleasant situations arise, we request to flag it to us in order to evaluate the situation.

Text source: Swahili New Testament, public domain.

This project is based on delivering free-of-charge the Word of the Lord in all the world by using electronic means. If you want to contact us, you can do this by writing to the following e-mail: bible-study.xyz@hotmail.com


SELECT VERSION

COMPARE WITH OTHER BIBLES