Bible Study: FrontPage




 

Marko, Chapter 8

Bible Study - Marko 8 - Swahili - Swahili New Testament - Web
 
 
 
Comment!       Comment Disqus!
  
1. Wakati huo umati mkubwa wa watu ulikusanyika tena, na hawakuwa na chakula. Basi, Yesu akawaita wanafunzi wake, akawaambia,
  
2. "Nawahurumia watu hawa kwa sababu wamekuwa nami kwa muda wa siku tatu, wala hawana chakula.
  
3. Nikiwaacha waende nyumbani wakiwa na njaa watazimia njiani, maana baadhi yao wametoka mbali."
  
4. Wanafunzi wake wakamwuliza, "Hapa nyikani itapatikana wapi mikate ya kuwashibisha watu hawa wote?"
  
5. Yesu akawauliza, "Mnayo mikate mingapi?" Nao wakamjibu, "Saba."
  
6. Basi, akawaamuru watu wakae chini. Akaitwaa ile mikate saba, akamshukuru Mungu, akaimega, akawapa wanafunzi wake wawagawie watu,nao wakawagawia.
  
7. Walikuwa pia na visamaki vichache. Yesu akavibariki, akaamuru vigawiwe watu vilevile.
  
8. Watu wakala, wakashiba. Wakaokota mabaki yaliyosalia wakajaza makapu saba.
  
9. Nao waliokula walikuwa watu wapatao elfu nne. Yesu akawaaga,
  
10. na mara akapanda mashua pamoja na wanafunzi wake, akaenda wilaya ya Dalmanutha.
  
11. Mafarisayo walikuja, wakaanza kujadiliana na Yesu. Kwa kumjaribu, wakamtaka awafanyie ishara kuonyesha anayo idhini kutoka mbinguni.
  
12. Yesu akahuzunika rohoni, akasema, "Mbona kizazi hiki kinataka ishara? Kweli nawaambieni, kizazi hiki hakitapewa ishara yoyote!"
  
13. Basi, akawaacha, akapanda tena mashua, akaanza safari kwenda ng`ambo ya pili ya ziwa.
  
14. Wanafunzi walikuwa wamesahau kuchukua mikate; walikuwa na mkate mmoja tu katika mashua.
  
15. Yesu akawaonya, "Angalieni sana! Jihadharini na chachu ya Mafarisayo na chachu ya Herode."
  
16. Wanafunzi wakaanza kujadiliana wao kwa wao, "Anasema hivyo kwa kuwa hatuna mikate."
  
17. Yesu alitambua hayo, akawaambia, "Mbona mnajadiliana juu ya kutokuwa na mikate? Je, bado hamjafahamu, wala hamjaelewa? Je, mioyo yenuimeshupaa?
  
18. Je, Mnayo macho na hamwoni? Mnayo masikio na hamsikii? Je, hamkumbuki
  
19. wakati ule nilipoimega ile mikate mitano na kuwapa watu elfu tano? Mlikusanya vikapu vingapi vya mabaki ya makombo?" Wakamjibu, "Kumi naviwili."
  
20. "Na nilipoimega ile mikate saba na kuwapa watu elfu nne, mlikusanya makapu mangapi ya makombo?" Wakamjibu, "Saba."
  
21. Basi, akawaambia, "Na bado hamjaelewa?"
  
22. Yesu alifika Bethsaida pamoja na wanafunzi wake. Huko watu wakamletea kipofu mmoja, wakamwomba amguse.
  
23. Yesu akamshika mkono huyo kipofu, akampeleka nje ya kijiji. Akamtemea mate machoni, akamwekea mikono, akamwuliza, "Je, unawezakuona kitu?"
  
24. Huyo kipofu akatazama, akasema, "Ninawaona watu wanaoonekana kama miti inayotembea."
  
25. Kisha Yesu akamwekea tena mikono machoni, naye akakaza macho, uwezo wake wa kuona ukamrudia, akaona kila kitu sawasawa.
  
26. Yesu akamwambia aende zake nyumbani na kumwamuru, "Usirudi kijijini!"
  
27. Kisha Yesu na wanafunzi wake walikwenda katika vijiji vya Kaisarea Filipi. Walipokuwa njiani, Yesu aliwauliza wanafunzi wake, "Watuwanasema mimi ni nani?"
  
28. Wakamjibu, "Wengine wanasema wewe ni Yohane Mbatizaji, wengine Eliya na wengine mmojawapo wa manabii."
  
29. Naye akawauliza, "Na ninyi je, mnasema mimi ni nani?" Petro akamjibu, "Wewe ndiwe Kristo."
  
30. Kisha Yesu akawaonya wasimwambie mtu yeyote habari zake.
  
31. Yesu alianza kuwafundisha wanafunzi wake: "Ni lazima Mwana wa Mtu apatwe na mateso mengi na kukataliwa na wazee na makuhani wakuu nawalimu wa Sheria. Atauawa na baada ya siku tatu atafufuka."
  
32. Yesu aliwaambia jambo hilo waziwazi. Basi, Petro akamchukua kando, akaanza kumkemea.
  
33. Lakini Yesu akageuka, akawatazama wanafunzi wake, akamkemea Petro akisema, "Ondoka mbele yangu, Shetani! Fikira zako si za kimungu ilani za kibinadamu!"
  
34. Kisha akauita umati wa watu pamoja na wanafunzi wake, akawaambia, "Mtu yeyote akitaka kuwa mfuasi wangu, lazima ajikane mwenyewe,auchukue msalaba wake, anifuate.
  
35. Maana mtu anayetaka kuyaokoa maisha yake mwenyewe, atayapoteza, lakini mtu atakayepoteza maisha yake kwa ajili yangu na kwa ajili yaHabari Njema, atayaokoa.
  
36. Je, kuna faida gani mtu kuupata ulimwengu wote na kuyapoteza maisha yake?
  
37. Ama mtu atatoa kitu gani badala ya maisha yake?
  
38. Mtu yeyote katika kizazi hiki kiovu na kisichomjali Mungu anayenionea aibu mimi na mafundisho yangu, Mwana wa Mtu atamwonea aibumtu huyo wakati atakapokuja katika utukufu wa Baba yake pamoja namalaika watakatifu."


Search in:
Terms:

Vote and Comment on Facebook:Recommend This Page:
Post on Facebook Add to your del.icio.us Digg this story StumbleUpon Twitter Google Plus Post on Tumblr Add to Reddit Pin this story Linkedin Google Bookmark Blogger
Insert Your Personal Insight:

Please do not make mean comments and follow the biblical and spiritual character of this forum. If, however unpleasant situations arise, we request to flag it to us in order to evaluate the situation.

Text source: Swahili New Testament, public domain.

This project is based on delivering free-of-charge the Word of the Lord in all the world by using electronic means. If you want to contact us, you can do this by writing to the following e-mail: bible-study.xyz@hotmail.com


SELECT VERSION

COMPARE WITH OTHER BIBLES