Bible Study: FrontPage




 

Mathayo, Chapter 26

Bible Study - Mathayo 26 - Swahili - Swahili New Testament - Web
 
 
 
Comment!       Comment Disqus!
  
1. Kulipopambazuka, makuhani wakuu wote na wazee wa watu walifanya mashauri juu ya Yesu wapate kumwua.
  
2. Wakamfunga pingu, wakamchukua, wakamkabidhi kwa Pilato, mkuu wa mkoa.
  
3. Hapo, Yuda ambaye ndiye aliyemsaliti, alipoona kwamba wamekwisha mhukumu Yesu, akajuta, akawarudishia makuhani wakuu zile sarafuthelathini za fedha.
  
4. Akawaambia, "Nimekosa kwa kumtoa mtu asiye na hatia auawe." Lakini wao wakasema, "Yatuhusu nini sisi? Hilo ni shauri lako."
  
5. Naye akazitupa zile fedha Hekaluni, akatoka nje, akaenda akajinyonga.
  
6. Makuhani wakuu wakazichukua zile fedha, wakasema, "Haifai kuziweka katika hazina ya Hekalu kwa maana ni fedha za damu."
  
7. Basi, wakashauriana, wakazitumia kununua shamba la mfinyanzi liwe mahali pa kuzika wageni.
  
8. Ndiyo maana mpaka leo shamba hilo linaitwa Shamba la Damu.
  
9. Hivyo maneno ya nabii Yeremia yakatimia: "Walizichukua sarafu thelathini za fedha, thamani ya yule ambaye watu wa Israeli walipangabei,
  
10. wakanunua nazo shamba la mfinyanzi, kama Bwana alivyoniagiza."
  
11. Yesu alisimamishwa mbele ya mkuu wa mkoa. Basi, mkuu wa mkoa akamwuliza, "Je, wewe ndiwe Mfalme wa Wayahudi?" Yesu akamwambia,"Wewe umesema."
  
12. Lakini makuhani wakuu na wazee walipokuwa wanamshtaki, hakujibu neno.
  
13. Hivyo Pilato akamwuliza, "Je, husikii mashtaka hayo yote wanayotoa juu yako?"
  
14. Lakini Yesu hakumjibu hata neno moja; hata huyo mkuu wa mkoa akashangaa sana.
  
15. Ilikuwa kawaida wakati wa Sikukuu ya Pasaka mkuu wa mkoa kuwafungulia Wayahudi mfungwa mmoja waliyemtaka.
  
16. Wakati huo kulikuwa na mfungwa mmoja, jina lake Baraba.
  
17. Hivyo, watu walipokusanyika pamoja, Pilato akawauliza, "Mwataka nimfungue yupi kati ya wawili hawa, Baraba*fq* ama Yesu aitwaeKristo?"
  
18. Alisema hivyo maana alijua wazi kwamba walimleta kwake kwa sababu ya wivu.
  
19. Pilato alipokuwa amekaa katika kiti cha hukumu, mke wake akampelekea ujumbe: "Usijitie katika shauri la mtu huyu mwema, maana leonimeteseka sana katika ndoto kwa sababu yake."
  
20. Lakini makuhani wakuu na wazee wakawashawishi watu waombe Baraba afunguliwe na Yesu auawe.
  
21. Mkuu wa mkoa akawauliza, "Ni yupi kati ya hawa wawili mnayetaka nimfungue?" Wakamjibu, "Baraba!"
  
22. Pilato akawauliza, "Sasa, nifanye nini na Yesu aitwaye Kristo?" Wote wakasema, "Asulubiwe!"
  
23. Pilato akauliza, "Kwa nini? Amefanya kosa gani?" Wao wakazidi kupaaza sauti: "Asulubiwe!"
  
24. Basi, Pilato alipotambua kwamba hafanikiwi chochote na kwamba maasi yalikuwa yanaanza, alichukua maji, akanawa mikono mbele ya ule umatiwa watu, akasema, "Mimi sina lawama juu ya kifo cha mtu huyu; shaurilenu wenyewe."
  
25. Watu wote wakasema, "Damu yake na iwe juu yetu na juu ya watoto wetu!"
  
26. Hapo Pilato akawafungulia Baraba kutoka gerezani, lakini akamtoa Yesu asulubiwe.
  
27. Kisha askari wa mkuu wa mkoa wakamwingiza Yesu ndani ya ikulu, wakamkusanyikia kikosi kizima.
  
28. Wakamvua nguo zake, wakamvika joho la rangi nyekundu.
  
29. Kisha wakasokota taji ya miiba, wakamvika kichwani, wakamwekea pia mwanzi katika mkono wake wa kulia. Wakapiga magoti mbele yake,wakamdhihaki wakisema, "Shikamoo mfalme wa Wayahudi!"
  
30. Wakamtemea mate, wakauchukua ule mwanzi, wakampiga nao kichwani.
  
31. Baada ya kumdhihaki, wakamvua lile joho, wakamvika nguo zake, kisha wakampeleka kumsulubisha.
  
32. Walipokuwa wakienda, wakamkuta mtu mmoja jina lake Simoni, mwenyeji wa Kurene, wakamlazimisha kuuchukua msalaba wake Yesu.
  
33. Walipofika mahali paitwapo Golgotha, maana yake, "Mahali pa Fuvu la kichwa,"
  
34. wakampa mchanganyiko wa divai na nyongo. Lakini Yesu alipoonja akakataa kunywa.
  
35. Walimsulubisha, kisha wakagawana mavazi yake kwa kuyapigia kura.
  
36. Wakaketi, wakawa wanamchunga.
  
37. Juu ya kichwa chake wakaweka shtaka dhidi yake lilioandikwa, "Huyu ni Yesu, Mfalme wa Wayahudi."
  
38. Wanyang`anyi wawili walisulubishwa pia pamoja naye, mmoja upande wa kushoto na mwingine upande wa kulia.
  
39. Watu waliokuwa wanapita mahali hapo walimtukana wakitikisa vichwa vyao na kusema,
  
40. "Wewe! Si ulijidai kulivunja Hekalu na kulijenga kwa siku tatu? Sasa jiokoe mwenyewe. Kama wewe ni Mwana wa Mungu, basi shuka msalabani!"
  
41. Hali kadhalika na makuhani wakuu pamoja na walimu wa Sheria na wazee walimdhihaki wakisema,
  
42. "Aliwaokoa wengine, lakini kujiokoa mwenyewe hawezi! Eti yeye ni mfalme wa Wayahudi! Basi, sasa na ashuke msalabani, nasi tutamwamini.
  
43. Alimtumainia Mungu na kusema eti yeye ni Mwana wa Mungu; basi, Mungu na amwokoe kama anamtaka."
  
44. Hali kadhalika na wale waliosulubiwa pamoja naye wakamtukana.
  
45. Tangu saa sita mchana mpaka saa tisa, nchi yote ikawa katika giza.
  
46. Mnamo saa tisa Yesu akalia kwa sauti kubwa, "Eli, Eli, lema sabakthani?" Maana yake, "Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?"
  
47. Lakini wale waliosimama pale waliposikia hivyo wakasema, "Anamwita Eliya."
  
48. Mmoja wao akakimbia, akachukua sifongo, akaichovya katika siki, akaiweka juu ya mwanzi, akampa anywe.
  
49. Wengine wakasema, "Acha tuone kama Eliya anakuja kumwokoa."
  
50. Basi, Yesu akalia tena kwa sauti kubwa, akakata roho.
  
51. Hapo pazia la Hekalu likapasuka vipande viwili, toka juu mpaka chini; nchi ikatetemeka; miamba ikapasuka;
  
52. makaburi yakafunguka na watu wengi wa Mungu waliokufa wakafufuliwa;
  
53. nao, baada ya kufufuka kwake, wakatoka makaburini, wakaingia katika Mji Mtakatifu, wakaonekana na watu wengi.
  
54. Basi, jemadari na wale waliokuwa wakimlinda Yesu walipoona tetemeko la ardhi na yale mambo yaliyotukia, wakaogopa sana, wakasema, "Hakikamtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu."
  
55. Mahali hapo walikuwapo wanawake wengi wakitazama kwa mbali. Hao ndio wale waliomfuata Yesu kutoka Galilaya wakimtumikia.
  
56. Miongoni mwao walikuwa Maria Magdalene, Maria mama yao Yakobo na Yosefu, pamoja na mama yao wana wa Zebedayo.
  
57. Ilipokuwa jioni, akaja mtu mmoja tajiri mwenyeji wa Armathaya, jina lake Yosefu. Yeye pia alikuwa mwanafunzi wa Yesu.
  
58. Akamwendea Pilato, akaomba apewe mwili wa Yesu. Basi, Pilato akaamuru apewe.
  
59. Yosefu akauchukua ule mwili akauzungushia sanda safi ya kitani,
  
60. akauweka ndani ya kaburi lake jipya alilokuwa amelichonga katika mwamba. Kisha akavingirisha jiwe kubwa mbele ya mlango wa kaburi,akaenda zake.
  
61. Maria Magdalene na yule Maria mwingine walikuwa wameketi kulielekea kaburi.
  
62. Kesho yake, yaani siku iliyofuata ile ya Maandalio, makuhani wakuu na Mafarisayo walimwendea Pilato,
  
63. Wakasema, "Mheshimiwa, tunakumbuka kwamba yule mdanganyifu alisema kabla ya kufa ati, `Baada ya siku tatu nitafufuka.`
  
64. Kwa hiyo amuru kaburi lilindwe mpaka siku ya tatu ili wanafunzi wake wasije wakamwiba na kuwaambia watu kwamba amefufuka. Uongo huu wamwisho utakuwa mbaya kuliko ule wa awali."
  
65. Pilato akawaambia, "Haya, mnao walinzi; nendeni mkalinde kadiri mjuavyo."
  
66. Basi, wakaenda, wakalilinda kaburi, wakatia mhuri juu ya lile jiwe na kuacha hapo askari walinzi.


Search in:
Terms:

Vote and Comment on Facebook:Recommend This Page:
Post on Facebook Add to your del.icio.us Digg this story StumbleUpon Twitter Google Plus Post on Tumblr Add to Reddit Pin this story Linkedin Google Bookmark Blogger
Insert Your Personal Insight:

Please do not make mean comments and follow the biblical and spiritual character of this forum. If, however unpleasant situations arise, we request to flag it to us in order to evaluate the situation.

Text source: Swahili New Testament, public domain.

This project is based on delivering free-of-charge the Word of the Lord in all the world by using electronic means. If you want to contact us, you can do this by writing to the following e-mail: bible-study.xyz@hotmail.com


SELECT VERSION

COMPARE WITH OTHER BIBLES