1. Kisha nikaona mnyama mmoja akitoka baharini. Alikuwa na vichwa saba na pembe kumi, na kila pembe ilikuwa na taji. Jina la kashfa lilikuwalimeandikwa juu ya vichwa hivyo.
2. Mnyama huyo niliyemwona alikuwa kama chui; miguu yake ilikuwa kama ya dubu, na kinywa chake kama cha simba. Lile joka likampa huyo mnyamanguvu yake, kiti chake cha enzi na uwezo mkuu.
3. Kichwa kimojawapo cha huyo mnyama kilionekana kama kilikwisha jeruhiwa vibaya sana, lakini jeraha hilo lilikuwa limepona. Dunianzima ilishangazwa na huyo mnyama na kumfuata.
4. Watu wote wakaliabudu lile joka kwa sababu lilimpa huyo mnyama uwezo wake. Wakamwabudu pia huyo mnyama wakisema, "Nani aliye kama huyumnyama? Ni nani awezaye kupigana naye?"
5. Kisha huyo mnyama akaruhusiwa kusema maneno ya kujigamba na kumkufuru Mungu; akaruhusiwa kuwa na mamlaka kwa muda wa miezi arobaini namiwili.
6. Basi, akaanza kumtukana Mungu, kulitukana jina lake, makao yake, na wote wakaao mbinguni.
7. Aliruhusiwa kuwapiga vita na kuwashinda watu wa Mungu. Alipewa mamlaka juu ya watu wa kila kabila, ukoo, lugha na taifa.
8. Wote waishio duniani watamwabudu isipokuwa tu wale ambao majina yao yameandikwa tangu mwanzo wa ulimwengu katika kitabu cha uzima chaMwanakondoo aliyechinjwa.
9. "Aliye na masikio, na asikie!
10. Waliokusudiwa kuchukuliwa mateka lazima watatekwa; waliokusudiwa kuuawa kwa upanga lazima watauawa kwa upanga. Kutokana na hayo nilazima watu wa Mungu wawe na uvumilivu na imani."
11. Kisha nikamwona mnyama mwingine anatoka ardhini. Alikuwa na pembe mbili kama pembe za kondoo, na aliongea kama joka.
12. Alikuwa na mamlaka kamili kutoka kwa yule mnyama wa kwanza, na akautumia uwezo huo mbele ya huyo mnyama. Akailazimisha dunia yote nawote waliomo humo kumwabudu huyo mnyama wa kwanza ambaye alikuwa najeraha la kifo lililokuwa limepona.
13. Basi, huyu mnyama wa pili akafanya miujiza mikubwa hata akasababisha moto kutoka mbinguni ushuke duniani mbele ya watu.
14. Aliwapotosha wakazi wa dunia kwa miujiza hiyo aliyojaliwa kutenda mbele ya mnyama wa kwanza. Aliwaambia wakazi wa dunia watengenezesanamu kwa heshima ya yule mnyama aliyekuwa amejeruhiwa kwa upangalakini akaishi tena.
15. Kisha alijaliwa kuipulizia uhai hiyo sanamu ya yule mnyama wa kwanza, hata ikaweza kuongea na kuwaua watu wote ambao hawakuiabudu.
16. Aliwalazimisha wote, wadogo na wakubwa, matajiri na maskini, watu huru na watumwa, watiwe alama juu ya mikono yao ya kulia au juu yapaji za nyuso zao.
17. Akapiga marufuku mtu yeyote kununua au kuuza kitu isipokuwa tu mtu aliyetiwa alama hiyo, yaani jina la yule mnyama au tarakimu ya jinahilo.
18. Hapa ni lazima kutumia ujasiri! Mwenye akili anaweza kufafanua maana ya tarakimu ya mnyama huyo, maana ni tarakimu yenye maana ya mtufulani. Tarakimu hiyo ni mia sita sitini na sita.
|