Bible Study: FrontPage




 

1 Mambo ya Nyakati, Chapter 20

Bible Study - 1 Mambo ya Nyakati 20 - Swahili - Swahili Union Bible - Web
 
 
 
Comment!       Comment Disqus!
  
1. Hata ikawa, mwanzo wa mwaka mpya, wakati watokapo wafalme kwenda vitani, Yoabu akawaongoza mashujaa wa jeshi, akaiteka nyara nchi ya wana wa Amoni, akaja akauhusuru Raba. Lakini Daudi akakaa Yerusalemu. Naye Yoabu akaupiga Raba akauangamiza.
  
2. Kisha Daudi akamtwalia mfalme wao taji toka kichwani pake, akaona ya kwamba uzani wake ni talanta ya dhahabu, na kulikuwa na vito vya thamani ndani yake; akavikwa Daudi kichwani; akazitoa nyara za mji, nyingi sana.
  
3. Na hao watu waliokuwamo akawatoa, akawakata-kata kwa misumeno, na kwa sululu za chuma, na kwa mashoka. Ndivyo alivyofanya Daudi kwa miji yote ya wana wa Amoni. Nao wakarudi Yerusalemu Daudi na watu wote.
  
4. Ikawa baada ya hayo, kulitokea vita na Wafilisti huko Gobu; ndipo Sibekai, Mhushathi, alipomwua Safu, mmojawapo wa Warefai; nao wakashindwa.
  
5. Kulikuwa na vita tena na Wafilisti; na Elhanani, mwana wa Yairi akamwua Lahmi nduguye Goliathi, Mgiti ,ambaye mti wa mkuki wake ulikuwa kama mti wa mfumaji.
  
6. Kulikuwa na vita tena huko Gathi; ambapo palikuwa na mtu mrefu sana, mwenye vidole vya mikono na miguu ishirini na vinne, kila mguu sita, na kila mkono sita; naye alizaliwa na Mrefai.
  
7. Naye huyo alipowatukana Israeli, Yonathani, mwana wa Shama, nduguye Daudi, akamwua.
  
8. Hao walizaliwa kwake huyo Mrefai wa Gathi,nao wakaanguka kwa mkono wa Daudi , na kwa mkono wa watumishi wake.


Search in:
Terms:

Vote and Comment on Facebook:Recommend This Page:
Post on Facebook Add to your del.icio.us Digg this story StumbleUpon Twitter Google Plus Post on Tumblr Add to Reddit Pin this story Linkedin Google Bookmark Blogger
Insert Your Personal Insight:

Please do not make mean comments and follow the biblical and spiritual character of this forum. If, however unpleasant situations arise, we request to flag it to us in order to evaluate the situation.

Text source: This text is in the public domain, downloaded from http://www.unboundbible.org, compiled by biblephone2008@gmail.com.

This project is based on delivering free-of-charge the Word of the Lord in all the world by using electronic means. If you want to contact us, you can do this by writing to the following e-mail: bible-study.xyz@hotmail.com


SELECT VERSION

COMPARE WITH OTHER BIBLES