Bible Study: FrontPage




 

2 Mambo ya Nyakati, Chapter 27

Bible Study - 2 Mambo ya Nyakati 27 - Swahili - Swahili Union Bible - Web
 
 
 
Comment!       Comment Disqus!
  
1. Yothamu alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala; akatawala katika Yerusalemu miaka kumi na sita; na jina la mamaye aliitwa Yerusha binti Sadoki.
  
2. Akafanya yaliyo ya adili machoni pa Bwana, sawasawa na yote aliyoyafanya Uzia babaye; isipokuwa hakuingia hekaluni mwa Bwana. Lakini watu walikuwa wakali kufanya maovu.
  
3. Ndiye aliyelijenga lango la juu la nyumba ya Bwana, na juu ya ukuta wa Ofeli akajenga sana.
  
4. Tena akajenga miji katika milima ya Yuda, na mwituni akajenga ngome na minara.
  
5. Kisha akapigana na mfalme wa wana wa Amoni, akawashinda. Na wana wa Amoni wakampa mwaka ule ule talanta mia za fedha, na kori elfu kumi za ngano, na elfu kumi za shayiri. Hayo ndiyo waliyomtolea wana wa Amoni, mwaka wa pili pia, na mwaka wa tatu.
  
6. Basi Yothamu akawa na nguvu, kwa kuwa alizitengeneza njia zake mbele za Bwana, Mungu wake.
  
7. Na mambo yote ya Yothamu yaliyosalia, na vita vyake vyote, na njia zake, tazama, yameandikwa katika kitabu cha wafalme wa Israeli na Yuda.
  
8. Alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala; akatawala miaka kumi na sita huko Yerusalemu.
  
9. Yothamu akalala na babaze, wakamzika katika mji wa Daudi; na Ahazi mwanawe akatawala mahali pake.


Search in:
Terms:

Vote and Comment on Facebook:Recommend This Page:
Post on Facebook Add to your del.icio.us Digg this story StumbleUpon Twitter Google Plus Post on Tumblr Add to Reddit Pin this story Linkedin Google Bookmark Blogger
Insert Your Personal Insight:

Please do not make mean comments and follow the biblical and spiritual character of this forum. If, however unpleasant situations arise, we request to flag it to us in order to evaluate the situation.

Text source: This text is in the public domain, downloaded from http://www.unboundbible.org, compiled by biblephone2008@gmail.com.

This project is based on delivering free-of-charge the Word of the Lord in all the world by using electronic means. If you want to contact us, you can do this by writing to the following e-mail: bible-study.xyz@hotmail.com


SELECT VERSION

COMPARE WITH OTHER BIBLES