Bible Study: FrontPage




 

Mhubiri, Chapter 1

Bible Study - Mhubiri 1 - Swahili - Swahili Union Bible - Web
 
 
 
Comment!       Comment Disqus!
  
1. Maneno ya Mhubiri mwana wa Daudi,mfalme katika Yerusalemu.
  
2. Mhubiri asema, Ubatili mtupu, ubatili mtupu, mambo yote ni ubatili.
  
3. Mtu ana faida gani ya kazi yake yote aifanyayo chini ya jua?
  
4. Kizazi huenda, kizazi huja; nayo dunia hudumu daima.
  
5. Jua lachomoza, na jua lashuka, na kufanya haraka kwenda mahali pa maawio yake.
  
6. Upepo huvuma kusi, hugeuka kuwa kaskazi; hugeuka daima katika mwendo wake, na upepo huyarudia mazunguko yake.
  
7. Mito yote huingia baharini, walakini bahari haijai; huko iendako mito, ndiko irudiko tena.
  
8. Mambo yote yamejaa uchovu usioneneka, jicho halishibi kuona, wala sikio halikinai kusikia.
  
9. Yaliyokuwako ndiyo yatakayokuwako; na yaliyotendeka ndiyo yatakayotendeka; wala jambo jipya hakuna chini ya jua.
  
10. Je! Kuna jambo lo lote ambalo watu husema juu yake, Tazama, ni jambo jipya? Limekwisha kuwako, tangu zamani za kale zilizokuwa kabla yetu sisi.
  
11. Hakuna kumbukumbu lo lote la vizazi vilivyotangulia; wala hakutakuwa na kumbukumbu lo lote la vizazi vitakavyokuja, miongoni mwao wale watakaofuata baadaye.
  
12. Mimi, Mhubiri, nalikuwa Mfalme wa Israeli katika Yerusalemu.
  
13. Nikatia moyo wangu ili kuyatafuta yote yanayotendeka chini ya mbingu, na kuyavumbua kwa hekima; ni taabu kubwa ambayo Mungu amewapa wanadamu, ili kutaabika ndani yake.
  
14. Nimeziona kazi zote zifanywazo chini ya jua; na, tazama, mambo yote ni ubatili na kujilisha upepo.
  
15. Yaliyopotoka hayawezi kunyoshwa, Wala yasiyokuwapo hayahesabiki.
  
16. Nikatafakari nikisema, Nimejipatia hekima nyingi kupita wote walionitangulia katika Yerusalemu; naam, moyo wangu umeona kwa wingi hekima na maarifa.
  
17. Nikatia moyo wangu ili kuijua hekima, na kujua wazimu na upumbavu; nikatambua ya kwamba hayo yote nayo ni kujilisha upepo.
  
18. Yaani, Katika wingi wa hekima mna wingi wa huzuni,Naye aongezaye maarifa huongeza masikitiko.


Search in:
Terms:

Vote and Comment on Facebook:Recommend This Page:
Post on Facebook Add to your del.icio.us Digg this story StumbleUpon Twitter Google Plus Post on Tumblr Add to Reddit Pin this story Linkedin Google Bookmark Blogger
Insert Your Personal Insight:

Please do not make mean comments and follow the biblical and spiritual character of this forum. If, however unpleasant situations arise, we request to flag it to us in order to evaluate the situation.

Text source: This text is in the public domain, downloaded from http://www.unboundbible.org, compiled by biblephone2008@gmail.com.

This project is based on delivering free-of-charge the Word of the Lord in all the world by using electronic means. If you want to contact us, you can do this by writing to the following e-mail: bible-study.xyz@hotmail.com


SELECT VERSION

COMPARE WITH OTHER BIBLES