|
|
Isaya, Chapter 4
1. Na siku hiyo wanawake saba watamshika mtu mume mmoja wakisema, Tutakula chakula chetu, na kuvaa nguo zetu wenyewe, lakini tuitwe tu kwa jina lako; utuondolee aibu yetu.
2. Siku hiyo chipukizi la Bwana litakuwa zuri, lenye utukufu, na matunda ya nchi yatakuwa mema sana, na kupendeza, kwa ajili ya Waisraeli wale waliookoka.
3. Tena itakuwa ya kwamba yeye aliyebaki katika Sayuni, na yeye aliyeachwa ndani ya Yerusalemu, ataitwa mtakatifu; yaani, kila mmoja aliyeandikwa miongoni mwa hao walio hai ndani ya Yerusalemu;
4. hapo Bwana atakapokuwa ameuosha uchafu wa hao binti za Sayuni na kuisafisha damu ya Yerusalemu kati yake, kwa roho ya hukumu na kwa roho ya kuteketeza.
5. Tena juu ya makao yote ya mlima Sayuni, na juu ya makusanyiko yake, Bwana ataumba wingu na moshi wakati wa mchana, na mwangaza wa miali ya moto wakati wa usiku; kwa maana juu ya utukufu wote itatandazwa sitara.
6. Kisha kutakuwa na hema kuwa uvuli wakati wa mchana kwa sababu ya hari, na kuwa mahali pa kukimbilia na kujificha wakati wa tufani na mvua.
|
|
Text source: This text is in the public domain, downloaded from http://www.unboundbible.org, compiled by biblephone2008@gmail.com.
|
| |
| This project is based on delivering free-of-charge the Word of the Lord in all the world by using electronic means. If you want to contact us, you can do this by writing to the following e-mail: bible-study.xyz@hotmail.com |
|
|
|
SELECT VERSION
COMPARE WITH OTHER BIBLES
|
|