Bible Study: FrontPage




 

Ayubu, Chapter 10

Bible Study - Ayubu 10 - Swahili - Swahili Union Bible - Web
 
 
 
Comment!       Comment Disqus!
  
1. Nafsi yangu inachoka na maisha yangu; Sitajizuia na kuugua kwangu; Nitanena kwa uchungu wa roho yangu.
  
2. Nitamwambia Mungu, Usinihukumie makosa; Nionyeshe sababu ya wewe kushindana nami.
  
3. Je! Ni vema kwako wewe kuonea, Na kuidharau kazi ya mikono yako, Na kuyaangazia mashauri ya waovu?
  
4. Je! Wewe una macho ya kimwili, Au je! Waona kama aonavyo binadamu?
  
5. Je! Siku zako ni kama siku za mtu, Au je! Miaka yako ni kama siku za mtu,
  
6. Hata ukauliza-uliza habari za uovu wangu, Na kuitafuta dhambi yangu,
  
7. Ujapojua ya kuwa mimi si mwovu; Wala hapana awezaye kuokoa na mkono wako?
  
8. Mikono yako imeniumba na kunifinyanga; Nawe utageuka na kuniangamiza?
  
9. Kumbuka, nakusihi ulivyonifinyanga kama vile udongo; Nawe, je! Utanirudisha uvumbini tena?
  
10. Je! Wewe hukunimimina kama maziwa, Na kunigandisha mfano wa jibini?
  
11. Umenivika ngozi na nyama, Na kuniunga pamoja kwa mifupa na mishipa.
  
12. Umenijazi uhai na upendeleo, Na maangalizi yako yameilinda roho yangu.
  
13. Lakini mambo haya uliyaficha moyoni mwako; Najua kuwa haya yamo nafsini mwako;
  
14. Nikifanya dhambi, ndipo waniangalia, Wala hutaniachilia na uovu wangu.
  
15. Mimi nikiwa mbaya, ole wangu! Nami nikiwa mwenye haki, walakini sitainua kichwa changu; Mimi nimejaa aibu Na kuyaangalia mateso yangu.
  
16. Kichwa changu kikijiinua, waniwinda kama simba; Tena wajionyesha kwangu kuwa wa ajabu.
  
17. Wewe warejeza upya hao mashahidi yako juu yangu, Na kasirani yako waiongeza juu yangu; Jeshi kwa jeshi juu yangu.
  
18. Kwa nini basi kunitoa tumboni? Ningekata roho, lisinione jicho lo lote.
  
19. Ningalikuwa kama mtu asiyekuwapo; Ningalichukuliwa kaburini kutoka tumboni.
  
20. Je! Siku zangu si chache? Acha basi, Usinisumbue, nipate ngaa kutuzwa moyo kidogo.
  
21. Kabla sijaenda huko ambako sitarudi kutoka huko tena, Ni hiyo nchi ya giza, giza tupu;
  
22. Ni nchi ya giza kuu, kama giza lenyewe lilivyo; Ni nchi ya giza tupu, isiyo na matengezo ya mambo yo yote, Nchi ambayo nuru yake ni kama giza.


Search in:
Terms:

Vote and Comment on Facebook:Recommend This Page:
Post on Facebook Add to your del.icio.us Digg this story StumbleUpon Twitter Google Plus Post on Tumblr Add to Reddit Pin this story Linkedin Google Bookmark Blogger
Insert Your Personal Insight:

Please do not make mean comments and follow the biblical and spiritual character of this forum. If, however unpleasant situations arise, we request to flag it to us in order to evaluate the situation.

Text source: This text is in the public domain, downloaded from http://www.unboundbible.org, compiled by biblephone2008@gmail.com.

This project is based on delivering free-of-charge the Word of the Lord in all the world by using electronic means. If you want to contact us, you can do this by writing to the following e-mail: bible-study.xyz@hotmail.com


SELECT VERSION

COMPARE WITH OTHER BIBLES