Bible Study: FrontPage




 

Ayubu, Chapter 18

Bible Study - Ayubu 18 - Swahili - Swahili Union Bible - Web
 
 
 
Comment!       Comment Disqus!
  
1. Ndipo Bildadi, Mshuhi, akajibu, na kusema,
  
2. Je! Hata lini utayategea maneno mitambo? Fikiri, kisha baadaye tutanena.
  
3. Twahesabiwa kuwa wanyama kwa sababu gani, Tena kuwa wanajisi machoni pako?
  
4. Wewe ujiraruaye mwenyewe katika hasira yako, Je! Dunia itaachwa kwa ajili yako wewe? Au jabali litaondolewa mahali pake?
  
5. Naam, mwanga wa waovu utazimika, Wala mwali wa moto wake hautang'aa.
  
6. Mwanga hemani mwake utakuwa giza, Nayo taa iliyo juu yake itazimishwa.
  
7. Hatua zake za nguvu zitasongwa, Na shauri lake mwenyewe litamwangusha chini.
  
8. Kwani ametupwa katika wavu na miguu yake mwenyewe, Naye huenda juu ya matanzi.
  
9. Tanzi litamshika kisigino chake, Na mtambo utamgwia.
  
10. Amefichiwa tanzi chini, Na mtego amewekewa njiani.
  
11. Matisho yatamtia hofu pande zote, Na kumfukuza karibu na visigino vyake.
  
12. Nguvu zake zitaliwa na njaa, Na msiba utakuwa tayari kwa kusita kwake.
  
13. Utakula via vya mwili wake, Naam, mzaliwa wa kwanza wa mauti atavila via vyake.
  
14. Atang'olewa katika hema yake aliyokuwa akiitumaini; Naye atapelekwa kwake mfalme wa utisho.
  
15. Ambacho si chake kitakaa katika hema yake; Kiberiti kitamwagwa juu ya makazi yake.
  
16. Chini, mizizi yake itakaushwa; Na juu, tawi lake litasinyaa.
  
17. Kumbukumbu lake litakoma katika nchi, Wala hatakuwa na jina mashambani.
  
18. Atakimbizwa kutoka mwangani hata gizani, Na kufukuzwa atoke duniani.
  
19. Hatakuwa na mwana wala mjukuu kati ya watu wake, Wala hatasalia mtu hapo alipokaa.
  
20. Hao wanaokaa magharibi watastaajabia siku yake, Kama vile wanaokaa mashariki walivyotiwa hofu.
  
21. Hakika ndivyo yalivyo makazi ya wapotovu, Na hapa ni mahali pake asiyemjua Mungu.


Search in:
Terms:

Vote and Comment on Facebook:Recommend This Page:
Post on Facebook Add to your del.icio.us Digg this story StumbleUpon Twitter Google Plus Post on Tumblr Add to Reddit Pin this story Linkedin Google Bookmark Blogger
Insert Your Personal Insight:

Please do not make mean comments and follow the biblical and spiritual character of this forum. If, however unpleasant situations arise, we request to flag it to us in order to evaluate the situation.

Text source: This text is in the public domain, downloaded from http://www.unboundbible.org, compiled by biblephone2008@gmail.com.

This project is based on delivering free-of-charge the Word of the Lord in all the world by using electronic means. If you want to contact us, you can do this by writing to the following e-mail: bible-study.xyz@hotmail.com


SELECT VERSION

COMPARE WITH OTHER BIBLES