Bible Study: FrontPage




 

Ayubu, Chapter 29

Bible Study - Ayubu 29 - Swahili - Swahili Union Bible - Web
 
 
 
Comment!       Comment Disqus!
  
1. Kisha Ayubu akaendelea na mithali yake, na kusema,
  
2. Laiti ningekuwa kama nilivyokuwa katika miezi ya kale, Kama katika siku hizo Mungu aliponilinda;
  
3. Hapo taa yake ilipomulika juu yangu kichwani, Nami nilitembea gizani kwa njia ya mwanga wake;
  
4. Kama nilivyokuwa katika siku zangu za kukomaa, Hapo siri ya Mungu ilipokuwa hemani mwangu;
  
5. Wakati Mwenyezi alipokuwa akali pamoja nami, Nao watoto wangu walipokuwa wakinizunguka;
  
6. Wakati hatua zangu zilipokuwa zikioshwa kwa siagi, Nalo jabali liliponimiminia mito ya mafuta!
  
7. Wakati nilipotoka kwenda mjini, hata langoni, Nilipokitengeza kiti changu katika njia kuu,
  
8. Hao vijana waliniona wakajificha, Nao wazee wakaniondokea na kusimama;
  
9. Wakuu wakanyamaa wasinene, Na kuweka mikono yao vinywani mwao;
  
10. Sauti yao masheki ilinyamaa, Na ndimi zao zilishikamana na makaakaa yao.
  
11. Maana sikio liliponisikia, ndipo likanibarikia; Na jicho liliponiona, likanishuhudia.
  
12. Kwa sababu nalimwokoa maskini aliyenililia; Yatima naye, na yule asiyekuwa na mtu wa kumsaidia.
  
13. Baraka yake yeye aliyekuwa karibu na kupotea ilinijia; Nikaufanya moyo wa mjane kuimba kwa furaha.
  
14. Nalijivika haki, ikanifunika, Adili yangu ilikuwa kama joho na kilemba.
  
15. Nalikuwa macho kwa kipofu, Nalikuwa miguu kwa aliyechechemea.
  
16. Nalikuwa baba kwa mhitaji, Na daawa ya mtu nisiyemjua naliichunguza.
  
17. Nami nilizivunja taya za wasio haki, Na kumpokonya mawindo katika meno yake.
  
18. Ndipo niliposema, Nitakufa ndani ya kioto changu, Nami nitaziongeza siku zangu kama mchanga;
  
19. Shina langu limeenea hata kufika majini, Na umande hukaa usiku kucha katika matawi yangu;
  
20. Utukufu wangu utakuwa mpya kwangu, Na uta wangu hurejezwa upya mkononi mwangu.
  
21. Watu walitega masikio kunisikiliza, na kungoja, Wakanyamaa kimya wapate sikia mashauri yangu.
  
22. Hawakunena tena baada ya kusikia maneno yangu; Matamko yangu yakadondoka juu yao.
  
23. Walikuwa wakiningojea kama kungojea mvua; Wakafunua vinywa vyao sana kama mvua ya masika.
  
24. Walipokata tamaa nikacheka nao; Na mwanga wa uso wangu hawakuuangusha.
  
25. Niliwachagulia njia, nikakaa kama mkuu wao. Nikakaa kama mfalme katika jeshi la askari, Mfano wa awafarijiye hao waombolezao.


Search in:
Terms:

Vote and Comment on Facebook:Recommend This Page:
Post on Facebook Add to your del.icio.us Digg this story StumbleUpon Twitter Google Plus Post on Tumblr Add to Reddit Pin this story Linkedin Google Bookmark Blogger
Insert Your Personal Insight:

Please do not make mean comments and follow the biblical and spiritual character of this forum. If, however unpleasant situations arise, we request to flag it to us in order to evaluate the situation.

Text source: This text is in the public domain, downloaded from http://www.unboundbible.org, compiled by biblephone2008@gmail.com.

This project is based on delivering free-of-charge the Word of the Lord in all the world by using electronic means. If you want to contact us, you can do this by writing to the following e-mail: bible-study.xyz@hotmail.com


SELECT VERSION

COMPARE WITH OTHER BIBLES