Bible Study: FrontPage




 

Ayubu, Chapter 32

Bible Study - Ayubu 32 - Swahili - Swahili Union Bible - Web
 
 
 
Comment!       Comment Disqus!
  
1. Basi hao watu watatu wakaacha kumjibu Ayubu, kwa sababu alikuwa mwenye haki machoni pake mwenyewe.
  
2. Ndipo zikawaka hasira za huyo Elihu mwana wa Barakeli, Mbuzi, katika jamaa ya Ramu, juu ya Ayubu, kwa sababu alikuwa amejipa haki mwenyewe zaidi ya Mungu.
  
3. Tena hasira zake ziliwaka juu ya hao rafiki zake watatu kwa sababu hawakupata jawabu, lakini wamemhukumia Ayubu makosa.
  
4. Basi huyo Elihu alikuwa anangoja ili anene na Ayubu, kwa sababu hao wengine walikuwa wazee kuliko yeye.
  
5. Hata Elihu alipoona kuwa hapana jawabu katika vinywa vya watu hao watatu, hasira zake ziliwaka.
  
6. Basi Elihu mwana wa Barakeli, Mbuzi, akajibu, na kusema, Mimi ni kijana, na ninyi ni wazee sana; Kwa hiyo nilijizuia, nisithubutu kuwaonyesha nionavyo.
  
7. Nilisema, Yafaa siku ziseme, Na wingi wa miaka ufundishe hekima.
  
8. Lakini imo roho ndani ya mwanadamu, Na pumzi za Mwenyezi huwapa akili.
  
9. Sio wakuu walio wenye akili, Wala sio wazee watambuao hukumu.
  
10. Basi nilisema, Nisikilizeni mimi; Mimi nami nitawaonyesha nionavyo.
  
11. Tazama, niliyangojea maneno yenu, Nilizisikiliza nisikie hoja zenu, Hapo mlipokitafuta mtakalonena.
  
12. Naam, niliwasikiza ninyi, Na tazama, hapana mmoja aliyemshinda Ayubu, Wala kumjibu maneno yake, kati yenu.
  
13. Jitunzeni msiseme, Sisi tumepata hekima; Mungu yumkini akamshinda, si mtu;
  
14. Kwa kuwa yeye hajayaelekeza maneno yake kwangu; Wala sitamjibu mimi kwa maneno yenu.
  
15. Wameshangaa, hawajibu tena; Hawana neno la kusema.
  
16. Na mimi, je! Ningoje, kwa sababu hawaneni, Kwa sababu wasimama kimya, wala wasijibu tena;
  
17. Mimi nami nitajibu sehemu yangu, Mimi nami nitaonyesha nionavyo.
  
18. Kwa kuwa nimejaa maneno; Roho iliyo ndani yangu hunihimiza.
  
19. Tazama, tumbo langu ni kama divai iliyozibwa; Kama viriba vipya li karibu na kupasuka.
  
20. Nitanena, ili nipate kutulia; Nitafunua midomo yangu na kujibu.
  
21. Tafadhali, nisiupendelee uso wa mtu; Wala sitajipendekeza kwa mtu ye yote.
  
22. Kwani mimi sijui kujipendekeza; Au Muumba wangu angeniondoa kwa upesi.


Search in:
Terms:

Vote and Comment on Facebook:Recommend This Page:
Post on Facebook Add to your del.icio.us Digg this story StumbleUpon Twitter Google Plus Post on Tumblr Add to Reddit Pin this story Linkedin Google Bookmark Blogger
Insert Your Personal Insight:

Please do not make mean comments and follow the biblical and spiritual character of this forum. If, however unpleasant situations arise, we request to flag it to us in order to evaluate the situation.

Text source: This text is in the public domain, downloaded from http://www.unboundbible.org, compiled by biblephone2008@gmail.com.

This project is based on delivering free-of-charge the Word of the Lord in all the world by using electronic means. If you want to contact us, you can do this by writing to the following e-mail: bible-study.xyz@hotmail.com


SELECT VERSION

COMPARE WITH OTHER BIBLES