Bible Study: FrontPage




 

Ayubu, Chapter 40

Bible Study - Ayubu 40 - Swahili - Swahili Union Bible - Web
 
 
 
Comment!       Comment Disqus!
  
1. Bwana akafuliza kumjibu Ayubu, na kusema,
  
2. Je! Mwenye hoja atashindana na Mwenyezi? Mwenye kujadiliana na Mungu, na ajibu yeye.
  
3. Ndipo Ayubu akamjibu Mungu, na kusema,
  
4. Tazama, mimi si kitu kabisa, nikujibu nini? Naweka mkono wangu kinywani pangu.
  
5. Nimenena mara moja, nami sitajibu; Naam, nimenena mara mbili, lakini sitaendelea zaidi.
  
6. Ndipo Bwana akamjibu Ayubu katika upepo wa kisulisuli, na kusema,
  
7. Jifunge viuno kama mwanamume, Mimi nitakuuliza neno, nawe niambie.
  
8. Je! Hata hukumu yangu utaibatilisha? Utanitia mimi hatiani, upate kuhesabiwa haki?
  
9. Au je! Wewe una mkono kama Mungu? Waweza kutoa ngurumo kwa sauti kama yeye?
  
10. Haya! Jivike sasa fahari na ukuu; Jipambe heshima na enzi.
  
11. Mwaga mafuriko ya hasira zako, Ukamtazame kila mtu mwenye kiburi, ukamdhili.
  
12. Mtazame kila mtu mwenye kiburi ukamshushe, Ukawakanyage waovu hapo wasimamapo.
  
13. Wafiche mavumbini pamoja, Wafunge nyuso zao mahali palipositirika.
  
14. Ndipo mimi nami nitazikiri habari zako, Ya kuwa mkono wako wa kuume waweza kukuokoa.
  
15. Mwangalie huyo kiboko, niliyemwumba pamoja nawe; Yeye hula nyasi kama vile ng'ombe,
  
16. Tazama basi, nguvu zake ni katika viuno vyake, Na uwezo wake u katika mishipa ya tumbo lake.
  
17. Yeye hutikisa mkia wake mfano wa mwerezi; Mishipa ya mapaja yake yanaungamana pamoja.
  
18. Mifupa yake ni kama mirija ya shaba; Mbavu zake ni kama vipande vya chuma.
  
19. Yeye ni mkuu wa njia za Mungu; Yeye aliyemfanya alimpa upanga wake.
  
20. Hakika milima humtolea chakula; Hapo wachezapo wanyama wote wa barani.
  
21. Hulala chini ya miti yenye vivuli, Mafichoni penye mianzi, na matopeni.
  
22. Hiyo miti yenye vivuli humfunika kwa vivuli vyao; Mierebi ya vijito humzunguka.
  
23. Tazama, mto ukifurika, yeye hatetemeki; Hujiona yu salama, ijapokuwa Yordani hufurika hata kinywani pake.
  
24. Je! Mtu ye yote atamnasa akiwa yu macho, Au, kumtoboa pua yake kwa mtego?


Search in:
Terms:

Vote and Comment on Facebook:Recommend This Page:
Post on Facebook Add to your del.icio.us Digg this story StumbleUpon Twitter Google Plus Post on Tumblr Add to Reddit Pin this story Linkedin Google Bookmark Blogger
Insert Your Personal Insight:

Please do not make mean comments and follow the biblical and spiritual character of this forum. If, however unpleasant situations arise, we request to flag it to us in order to evaluate the situation.

Text source: This text is in the public domain, downloaded from http://www.unboundbible.org, compiled by biblephone2008@gmail.com.

This project is based on delivering free-of-charge the Word of the Lord in all the world by using electronic means. If you want to contact us, you can do this by writing to the following e-mail: bible-study.xyz@hotmail.com


SELECT VERSION

COMPARE WITH OTHER BIBLES