Bible Study: FrontPage




 

Nehemia, Chapter 10

Bible Study - Nehemia 10 - Swahili - Swahili Union Bible - Web
 
 
 
Comment!       Comment Disqus!
  
1. Basi hawa ndio waliotia muhuri; Nehemia, ndiye Tirshatha, mwana wa Hakalia, na Sedekia;
  
2. Seraya, Azaria, Yeremia;
  
3. Pashuri, Amaria, Malkiya;
  
4. Hamshi, Shekania, Maluki;
  
5. Harimu, Meremothi, Obadia;
  
6. Danieli, Ginethoni, Baruki;
  
7. Meshulamu, Abiya, Miyamini;
  
8. Maazia, Bilgai, Shemaya; hao ndio waliokuwa makuhani.
  
9. Na Walawi; ndio, Yeshua, mwana wa Azania, Binui wa wana wa Henadadi, Kadmieli;
  
10. na ndugu zao, Shebania, Hodia, Kelita, Pelaya, Hanani;
  
11. Mika, Rehobu, Hashabia;
  
12. Zakuri, Sherebia, Shebania;
  
13. Hodia, Bani, Beninu;
  
14. Na wakuu wa watu; Paroshi, Pahath-Moabu, Elamu, Zatu, Bani;
  
15. Buni, Azgadi, Bebai;
  
16. Adonikamu, Bigwai, Adini;
  
17. Ateri, Hezakia, Azuri;
  
18. Hodia, Hashumu, Besai;
  
19. Harifu, Anathothi, Nobai;
  
20. Magpiashi, Meshulamu, Heziri;
  
21. Meshezabeli, Sadoki, Yadua;
  
22. Pelatia, Hanani, Anaya;
  
23. Hoshea, Hanania, Hashubu;
  
24. Haloheshi, Pilha, Shobeki;
  
25. Rehumu, Hashabna, Maaseya;
  
26. Ahia, Hanani, Anani;
  
27. Maluki, Harimu, na Baana.
  
28. Na watu waliosalia, makuhani, Walawi, mabawabu, waimbaji, Wanethini, na hao wote waliojitenga katika watu wa nchi kwa torati ya Mungu; wake zao, na wana wao, na binti zao, kila mwenye maarifa na akili;
  
29. wakaambatana na ndugu zao, wakuu wao, nao wakaingia katika laana na kiapo, ya kuwa wataiendea torati ya Mungu, iliyotolewa kwa mkono wa Musa, mtumishi wa Mungu, na kuziangalia, na kuzitenda, amri zote za Bwana, Bwana wetu, na hukumu zake na sheria zake;
  
30. wala tusiwaoze watu wa nchi binti zetu, wala kuwatwalia wana wetu binti zao;
  
31. tena watu wa nchi wakitembeza biashara, au chakula cho chote, siku ya sabato, tusinunue kwao siku ya sabato, au siku takatifu; tena kwamba tuuache mwaka wa saba, na madai ya kila deni.
  
32. Tena tukajifanyia maagizo, kujitoza mwaka kwa mwaka theluthi ya shekeli kwa huduma ya nyumba ya Mungu wetu;
  
33. kwa mikate ya wonyesho, na kwa sadaka ya unga ya daima, na kwa sadaka ya kuteketezwa ya daima, ya sabato, na ya siku za mwezi mpya, na ya sikukuu, tena kwa vitu vile vitakatifu, na kwa sadaka za dhambi, za kuwafanyia Israeli upatanisho, na kwa ajili ya kazi yote ya nyumba ya Mungu wetu.
  
34. Kisha tukapiga kura, makuhani, na Walawi, na watu, juu ya matoleo ya kuni, ili kuzileta nyumbani kwa Mungu wetu, kwa kadiri ya mbari za baba zetu, kwa nyakati zilizoamriwa, mwaka kwa mwaka, kukoka moto madhabahuni mwa Bwana, Mungu wetu, kama ilivyoandikwa katika torati;
  
35. tena kuleta malimbuko ya ardhi yetu, na malimbuko ya matunda yote ya miti ya namna zote, mwaka kwa mwaka, nyumbani kwa Bwana;
  
36. tena wazaliwa wa kwanza wa wana wetu, na wa wanyama wetu, kama ilivyoandikwa katika torati, na wazaliwa wa kwanza wa ng'ombe zetu na kondoo zetu, ili kuwaleta nyumbani mwa Mungu wetu, kwa makuhani watumikao nyumbani mwa Mungu wetu;
  
37. tena tuyalete malimbuko ya unga wetu, na sadaka zetu za kuinuliwa, na matunda ya miti ya namna zote, mvinyo, na mafuta, kwa makuhani, hapo vyumbani kwa nyumba ya Mungu wetu; na zaka za ardhi yetu kwa Walawi; kwa kuwa hao Walawi wazitwaa zaka mijini mwote mwa kulima kwetu.
  
38. Naye kuhani, mwana wa Haruni, atakuwako pamoja na Walawi, watwaapo zaka Walawi; nao Walawi wataipandisha zaka ya hizo zaka nyumbani kwa Mungu wetu, vyumbani, katika nyumba ya hazina.
  
39. Kwa kuwa wana wa Israeli na wana wa Lawi wataleta sadaka ya kuinuliwa ya nafaka, na mvinyo, na mafuta, vyumbani, kwa kuwa ndimo vilimo vyombo vya patakatifu, na makuhani watumikao, na mabawabu, na waimbaji; wala sisi hatutaiacha nyumba ya Mungu wetu.


Search in:
Terms:

Vote and Comment on Facebook:Recommend This Page:
Post on Facebook Add to your del.icio.us Digg this story StumbleUpon Twitter Google Plus Post on Tumblr Add to Reddit Pin this story Linkedin Google Bookmark Blogger
Insert Your Personal Insight:

Please do not make mean comments and follow the biblical and spiritual character of this forum. If, however unpleasant situations arise, we request to flag it to us in order to evaluate the situation.

Text source: This text is in the public domain, downloaded from http://www.unboundbible.org, compiled by biblephone2008@gmail.com.

This project is based on delivering free-of-charge the Word of the Lord in all the world by using electronic means. If you want to contact us, you can do this by writing to the following e-mail: bible-study.xyz@hotmail.com


SELECT VERSION

COMPARE WITH OTHER BIBLES