Bible Study: FrontPage




 

Mithali, Chapter 1

Bible Study - Mithali 1 - Swahili - Swahili Union Bible - Web
 
 
 
Comment!       Comment Disqus!
  
1. Mithali za Sulemani, mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli.
  
2. Kujua hekima na adabu; kutambua maneno ya ufahamu;
  
3. kufundishwa matendo ya busara, katika haki na hukumu na adili.
  
4. Kuwapa wajinga werevu, na kijana maarifa na hadhari;
  
5. mwenye hekima asikie na kuongezewa elimu, na mwenye ufahamu ayafikie mashauri yenye njia.
  
6. Kufahamu mithali na kitendawili, na maneno ya wenye hekima na mafumbo yao.
  
7. Kumcha Bwana ni chanzo cha maarifa, Bali wapumbavu hudharau hekima na adabu.
  
8. Mwanangu, yasikilize mafundisho ya baba yako, Wala usiiache sheria ya mama yako,
  
9. Kwa maana hayo yatakuwa kilemba cha neema kichwani pako, Na mikufu shingoni mwako.
  
10. Mwanangu, wenye dhambi wakikushawishi, Wewe usikubali.
  
11. Wakisema, Haya! Njoo pamoja nasi, Na tuvizie ili kumwaga damu; Tumwotee asiye na hatia, bila sababu;
  
12. Tuwameze hai kama kuzimu, Na wazima, kama wao washukao shimoni.
  
13. Tutapata mali yote ya thamani, Tutazijaza nyumba zetu mateka.
  
14. Wewe utashirikiana nasi; Tutakuwa na vitu vyote shirika.
  
15. Mwanangu, usiende njiani pamoja nao; Uzuie mguu wako usiende katika mapito yao.
  
16. Maana miguu yao huenda mbio maovuni, Nao hufanya haraka ili kumwaga damu.
  
17. Kwa kuwa mtego hutegwa bure, Mbele ya macho ya ndege ye yote.
  
18. Na hao hujiotea damu yao wenyewe, Hujinyemelea nafsi zao wenyewe.
  
19. Ndivyo zilivyo njia za kila mwenye tamaa ya mali; Huuondoa uhai wao walio nayo.
  
20. Hekima hupaza sauti yake katika njia kuu, Hutoa sauti yake katika viwanja;
  
21. Hulia penye mikutano mikubwa ya watu, Mahali pa kuyaingilia malango, Ndani ya mji hutamka maneno yake.
  
22. Enyi wajinga, hata lini mtapenda ujinga? Na wenye dharau kupenda dharau yao, Na wapumbavu kuchukia maarifa?
  
23. Geukeni kwa ajili ya maonyo yangu; Tazama, nitawamwagia roho yangu, Na kuwajulisheni maneno yangu.
  
24. Kwa kuwa nimeita, nanyi mkakataa; Nimeunyosha mkono wangu, asiangalie mtu;
  
25. Bali mmebatilisha shauri langu, Wala hamkutaka maonyo yangu;
  
26. Mimi nami nitacheka siku ya msiba wenu, Nitadhihaki hofu yenu ifikapo;
  
27. Hofu yenu ifikapo kama tufani, Na msiba wenu ufikapo kama kisulisuli, Dhiki na taabu zitakapowafikia.
  
28. Ndipo watakaponiita, lakini sitaitika; Watanitafuta kwa bidii, wasinione.
  
29. Kwa kuwa walichukia maarifa, Wala hawakuchagua kumcha Bwana.
  
30. Hawakukubali mashauri yangu, Wakayadharau maonyo yangu yote.
  
31. Kwa hiyo watakula matunda ya njia yao, Watashiba mashauri yao wenyewe.
  
32. Maana kurudi nyuma kwao wajinga kutawaua, Na kufanikiwa kwao wapumbavu kutawaangamiza.
  
33. Bali kila anisikilizaye atakaa salama, Naye atatulia bila kuogopa mabaya.


Search in:
Terms:

Vote and Comment on Facebook:Recommend This Page:
Post on Facebook Add to your del.icio.us Digg this story StumbleUpon Twitter Google Plus Post on Tumblr Add to Reddit Pin this story Linkedin Google Bookmark Blogger
Insert Your Personal Insight:

Please do not make mean comments and follow the biblical and spiritual character of this forum. If, however unpleasant situations arise, we request to flag it to us in order to evaluate the situation.

Text source: This text is in the public domain, downloaded from http://www.unboundbible.org, compiled by biblephone2008@gmail.com.

This project is based on delivering free-of-charge the Word of the Lord in all the world by using electronic means. If you want to contact us, you can do this by writing to the following e-mail: bible-study.xyz@hotmail.com


SELECT VERSION

COMPARE WITH OTHER BIBLES