Bible Study: FrontPage




 

Mithali, Chapter 15

Bible Study - Mithali 15 - Swahili - Swahili Union Bible - Web
 
 
 
Comment!       Comment Disqus!
  
1. Jawabu la upole hugeuza hasira; Bali neno liumizalo huchochea ghadhabu.
  
2. Ulimi wa mwenye hekima hutamka maarifa vizuri; Bali vinywa vya wapumbavu humwaga upumbavu.
  
3. Macho ya Bwana yako kila mahali; Yakimchunguza mbaya na mwema.
  
4. Ulimi safi ni mti wa uzima; Bali ukorofi wa ulimi huvunja moyo.
  
5. Mpumbavu hudharau kurudiwa na babaye; Bali yeye aangaliaye maonyo hupata busara.
  
6. Katika nyumba ya mwenye haki mna akiba nyingi; Bali mapato ya mtu mbaya huwa taabu tu.
  
7. Midomo ya mwenye haki hueneza maarifa; Bali moyo wa mpumbavu haufanyi hivyo.
  
8. Sadaka ya mtu mbaya ni chukizo kwa Bwana; Bali maombi ya mtu mnyofu ni furaha yake.
  
9. Njia ya mtu mbaya ni chukizo kwa Bwana; Bali humpenda mtu afuatiaye wema.
  
10. Adhabu kali ina yeye aiachaye njia; Naye achukiaye kukemewa atakufa.
  
11. Kuzimu na Uharibifu vi wazi mbele za Bwana; Si zaidi basi, mioyo ya wanadamu?
  
12. Mwenye mzaha hapendi kukaripiwa; Wala yeye hawaendei wenye hekima.
  
13. Moyo wa furaha huchangamsha uso; Bali kwa huzuni ya moyo roho hupondeka.
  
14. Moyo wa mwenye ufahamu hutafuta maarifa; Bali kinywa cha wapumbavu hula upumbavu.
  
15. Siku zote za mtu ateswaye ni mbaya; Bali ukunjufu wa moyo ni karamu ya daima.
  
16. Kuwa na mali chache pamoja na kumcha Bwana; Ni bora kuliko mali nyingi pamoja na taabu.
  
17. Chakula cha mboga penye mapendano; Ni bora kuliko ng'ombe aliyenona pamoja na kuchukiana.
  
18. Mtu wa hasira huchochea ugomvi; Bali asiye mwepesi wa hasira hutuliza mashindano.
  
19. Njia ya mtu mvivu ni kama boma la miiba; Bali mapito yao wenye unyofu hufanyika njia kuu.
  
20. Mwana mwenye hekima humfurahisha babaye; Bali mpumbavu humdharau mamaye.
  
21. Upumbavu ni furaha kwake aliyepungukiwa na akili; Bali mwenye ufahamu huunyosha mwenendo wake.
  
22. Pasipo mashauri makusudi hubatilika; Bali kwa wingi wa washauri huthibithika.
  
23. Mtu hulifurahia jibu la kinywa chake; Na neno linenwalo wakati wa kufaa ni jema kama nini!
  
24. Kwa mtu mwenye akili njia ya uhai huenda juu; Ili atoke katika kuzimu chini.
  
25. Bwana ataing'oa nyumba ya mwenye kiburi; Bali atauthibitisha mpaka wa mjane.
  
26. Mashauri mabaya ni chukizo kwa Bwana; Bali maneno yapendezayo ni safi.
  
27. Atamaniye faida huifadhaisha nyumba yake mwenyewe; Bali achukiaye zawadi ataishi.
  
28. Moyo wa mwenye haki hufikiri jinsi atakavyojibu; Bali kinywa cha wasio haki humwaga mabaya.
  
29. Bwana yu mbali na wasio haki; Bali huisikia sala ya mwenye haki.
  
30. Mng'ao wa macho huufurahisha moyo; Habari njema huinenepesha mifupa.
  
31. Sikio lisikilizalo lawama yenye uhai Litakaa kati yao wenye hekima.
  
32. Akataaye maonyo huidharau nafsi yake mwenyewe; Bali yeye asikilizaye lawama hujipatia ufahamu.
  
33. Kumcha Bwana ni maonyo ya hekima; Na kabla ya heshima hutangulia unyenyekevu.


Search in:
Terms:

Vote and Comment on Facebook:Recommend This Page:
Post on Facebook Add to your del.icio.us Digg this story StumbleUpon Twitter Google Plus Post on Tumblr Add to Reddit Pin this story Linkedin Google Bookmark Blogger
Insert Your Personal Insight:

Please do not make mean comments and follow the biblical and spiritual character of this forum. If, however unpleasant situations arise, we request to flag it to us in order to evaluate the situation.

Text source: This text is in the public domain, downloaded from http://www.unboundbible.org, compiled by biblephone2008@gmail.com.

This project is based on delivering free-of-charge the Word of the Lord in all the world by using electronic means. If you want to contact us, you can do this by writing to the following e-mail: bible-study.xyz@hotmail.com


SELECT VERSION

COMPARE WITH OTHER BIBLES