Bible Study: FrontPage




 

Mithali, Chapter 18

Bible Study - Mithali 18 - Swahili - Swahili Union Bible - Web
 
 
 
Comment!       Comment Disqus!
  
1. Ajitengaye na wenzake hutafuta matakwa yake mwenyewe; Hushindana na kila shauri jema.
  
2. Mpumbavu hapendezwi na ufahamu; Ila moyo wake udhihirike tu.
  
3. Ajapo asiye haki, huja dharau pia; Na pamoja na aibu huja lawama.
  
4. Maneno ya kinywa cha mtu ni kama maji ya vilindi; Kijito kibubujikacho; chemchemi ya hekima.
  
5. Kukubali uso wake asiye haki si vizuri; Wala kumpotosha mwenye haki hukumuni.
  
6. Midomo ya mpumbavu huingia katika fitina, Na kinywa chake huita mapigo.
  
7. Kinywa cha mpumbavu ni uharibifu wake, Na midomo yake ni mtego wa nafsi yake.
  
8. Maneno ya mchongezi ni kama vitoweo; Nayo hushukia pande za ndani za tumbo.
  
9. Yeye naye aliye mvivu katika kazi yake, Ni ndugu yake aliye mharabu.
  
10. Jina la Bwana ni ngome imara; Mwenye haki huikimbilia, akawa salama.
  
11. Mali ya mtu tajiri ni mji wake wa nguvu; Ni kama ukuta mrefu katika mawazo yake.
  
12. Kabla ya uharibifu moyo wa mwanadamu hujivuna; Na kabla ya heshima hutangulia unyenyekevu.
  
13. Yeye ajibuye kabla hajasikia, Ni upumbavu na aibu kwake.
  
14. Roho ya mtu itastahimili udhaifu wake; Bali roho iliyovunjika nani awezaye kuistahimili?
  
15. Moyo wa mwenye busara hupata maarifa; Na sikio la mwenye hekima hutafuta maarifa.
  
16. Zawadi ya mtu humpatia nafasi; Humleta mbele ya watu wakuu.
  
17. Ajiteteaye kwanza huonekana kuwa ana haki; Lakini jirani yake huja na kumchunguza.
  
18. Kura hukomesha mashindano; Hukata maneno ya wakuu.
  
19. Ndugu aliyechukizwa ni mgumu kuliko mji wa nguvu; Na mashindano ni kama mapingo ya ngome.
  
20. Tumbo la mtu litajazwa matunda ya kinywa chake; Atashiba mazao ya midomo yake.
  
21. Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yake.
  
22. Apataye mke apata kitu chema; Naye ajipatia kibali kwa Bwana.
  
23. Maskini hutumia maombi; Bali tajiri hujibu kwa ukali.
  
24. Ajifanyiaye rafiki wengi ni kwa uangamivu wake mwenyewe; Lakini yuko rafiki aambatanaye na mtu kuliko ndugu.


Search in:
Terms:

Vote and Comment on Facebook:Recommend This Page:
Post on Facebook Add to your del.icio.us Digg this story StumbleUpon Twitter Google Plus Post on Tumblr Add to Reddit Pin this story Linkedin Google Bookmark Blogger
Insert Your Personal Insight:

Please do not make mean comments and follow the biblical and spiritual character of this forum. If, however unpleasant situations arise, we request to flag it to us in order to evaluate the situation.

Text source: This text is in the public domain, downloaded from http://www.unboundbible.org, compiled by biblephone2008@gmail.com.

This project is based on delivering free-of-charge the Word of the Lord in all the world by using electronic means. If you want to contact us, you can do this by writing to the following e-mail: bible-study.xyz@hotmail.com


SELECT VERSION

COMPARE WITH OTHER BIBLES