Bible Study: FrontPage




 

Mithali, Chapter 20

Bible Study - Mithali 20 - Swahili - Swahili Union Bible - Web
 
 
 
Comment!       Comment Disqus!
  
1. Mvinyo hudhihaki, kileo huleta ugomvi; Na akosaye kwa vitu hivyo hana hekima.
  
2. Utisho wa mfalme ni kama ngurumo ya simba; Amkasirishaye huitendea dhambi nafsi yake.
  
3. Mtu kujitenga na ugomvi ni heshima kwake; Bali kila mpumbavu ataka kugombana.
  
4. Mtu mvivu hataki kulima wakati wa baridi; Hivyo wakati wa mavuno ataomba, hana kitu.
  
5. Mashauri ya moyoni ni kama kilindi; Lakini mtu mwenye ufahamu atayateka.
  
6. Wanadamu hutangaza kila mtu hisani yake mwenyewe; Bali mtu aliye mwaminifu, ni nani awezaye kumpata?
  
7. Mwenye haki aendaye katika unyofu wake, Watoto wake wabarikiwa baada yake.
  
8. Mfalme aketiye katika kiti cha hukumu, Huyapepeta mabaya yote kwa macho yake.
  
9. Nani awezaye kusema, Nimesafisha moyo wangu; Nimetakasika dhambi yangu?
  
10. Vipimo mbalimbali, na pishi mbalimbali, Vyote viwili ni chukizo kwa Bwana.
  
11. Hata mtoto hujijulisha kwa matendo yake; Kwamba kazi yake ni safi, kwamba ni adili.
  
12. Sikio lisikialo, na jicho lionalo, Bwana ndiye aliyeyafanya yote mawili.
  
13. Usipende usingizi usije ukawa maskini; Fumbua macho yako nawe utashiba chakula.
  
14. Haifai kitu, haifai kitu, asema mnunuzi; Lakini akiisha kwenda zake hujisifu.
  
15. Dhahabu iko, na marijani tele; Lakini midomo ya maarifa ni kito cha thamani.
  
16. Twaa nguo yake amdhaminiye mgeni; Mtoze rehani aliye mdhamini wa wageni.
  
17. Chakula cha uongo ni kitamu kwa mtu; Lakini halafu kinywa chake kitajaa changarawe.
  
18. Kila kusudi huthibitika kwa kushauriana; Na kwa shauri la akili fanya vita.
  
19. Mwenye kitango akisingizia hufunua siri; Basi, usishirikiane naye afunuaye midomo yake sana.
  
20. Amlaaniye babaye au mamaye, Taa yake itazimika katika giza kuu.
  
21. Urithi uliopatikana mwanzo kwa haraka, Mwisho wake, lakini, hautabarikiwa.
  
22. Usiseme, Mimi nitalipa mabaya; Mngojee Bwana, naye atakuokoa.
  
23. Vipimo mbalimbali ni chukizo kwa Bwana; Tena mizani ya hila si njema.
  
24. Mwenendo wa mtu watoka kwa Bwana; Basi, awezaje mtu kuelewa na njia yake?
  
25. Ni mtego, mtu aseme kwa haraka, Kitu hiki ni wakfu; Na baada ya kuweka nadhiri kuuliza-uliza habari.
  
26. Mfalme mwenye hekima huwapepeta wasio haki; Naye hulipitisha gurudumo la kupuria juu yao.
  
27. Pumzi ya mwanadamu ni taa ya Bwana; Hupeleleza yote yaliyomo ndani yake.
  
28. Fadhili na uaminifu humhifadhi mfalme, Na kiti chake cha enzi huthibitishwa kwa fadhili.
  
29. Fahari ya vijana ni nguvu zao, Na uzuri wa wazee ni kichwa chenye mvi.
  
30. Machubuko ya fimbo husafisha uovu, Na mapigo hufikilia ndani ya mtima.


Search in:
Terms:

Vote and Comment on Facebook:Recommend This Page:
Post on Facebook Add to your del.icio.us Digg this story StumbleUpon Twitter Google Plus Post on Tumblr Add to Reddit Pin this story Linkedin Google Bookmark Blogger
Insert Your Personal Insight:

Please do not make mean comments and follow the biblical and spiritual character of this forum. If, however unpleasant situations arise, we request to flag it to us in order to evaluate the situation.

Text source: This text is in the public domain, downloaded from http://www.unboundbible.org, compiled by biblephone2008@gmail.com.

This project is based on delivering free-of-charge the Word of the Lord in all the world by using electronic means. If you want to contact us, you can do this by writing to the following e-mail: bible-study.xyz@hotmail.com


SELECT VERSION

COMPARE WITH OTHER BIBLES