Bible Study: FrontPage




 

Mithali, Chapter 4

Bible Study - Mithali 4 - Swahili - Swahili Union Bible - Web
 
 
 
Comment!       Comment Disqus!
  
1. Wanangu, yasikilizeni mausia ya baba yenu, Tegeni masikio mpate kujua ufahamu.
  
2. Kwa kuwa nawapa mafundisho mazuri; Msiiache sheria yangu.
  
3. Maana nalikuwa mwana kwa baba yangu, Mpole, mpenzi wa pekee wa mama yangu.
  
4. Naye akanifundisha, akaniambia, Moyo wako uyahifadhi maneno yangu; Shika amri zangu ukaishi.
  
5. Jipatie hekima, jipatie ufahamu; usiusahau; Wala usiyakatae maneno ya kinywa changu.
  
6. Usimwache, naye atakuhifadhi; Umpende, naye atakulinda.
  
7. Bora hekima, basi jipatie hekima; Naam, kwa mapato yako yote jipatie ufahamu.
  
8. Umtukuze, naye atakukuza; Atakupatia heshima, ukimkumbatia.
  
9. Atakupa neema kuwa kilemba kichwani; Na kukukirimia taji ya uzuri.
  
10. Mwanangu, sikiliza, na kuzipokea kauli zangu; Na miaka ya maisha yako itakuwa mingi.
  
11. Nimekufundisha katika njia ya hekima; Nimekuongoza katika mapito ya unyofu.
  
12. Uendapo, hatua zako hazitadhiikika, Wala ukipiga mbio hutajikwaa.
  
13. Mkamate sana elimu, usimwache aende zake; Mshike, maana yeye ni uzima wako.
  
14. Usiingie katika njia ya waovu, Wala usitembee katika njia ya wabaya.
  
15. Jiepushe nayo, usipite karibu nayo, Igeukie mbali, ukaende zako.
  
16. Maana hawalali isipokuwa wametenda madhara; Huondolewa usingizi, ikiwa hawakumwangusha mtu.
  
17. Maana wao hula mkate wa uovu, Nao hunywa divai ya jeuri.
  
18. Bali njia ya wenye haki ni kama nuru ing'aayo, Ikizidi kung'aa hata mchana mkamilifu.
  
19. Njia ya waovu ni kama giza; Hawajui ni kitu gani kiwakwazacho.
  
20. Mwanangu, sikiliza maneno yangu; Tega sikio lako, uzisikie kauli zangu.
  
21. Zisiondoke machoni pako; Uzihifadhi ndani ya moyo wako.
  
22. Maana ni uhai kwa wale wazipatao, Na afya ya mwili wao wote.
  
23. Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.
  
24. Kinywa cha ukaidi ukitenge nawe, Na midomo ya upotovu uiweke mbali nawe.
  
25. Macho yako yatazame mbele, Na kope zako zitazame mbele yako sawasawa.
  
26. Ulisawazishe pito la mguu wako, Na njia zako zote zithibitike;
  
27. Usigeuke kwa kuume wala kwa kushoto; Ondoa mguu wako maovuni.


Search in:
Terms:

Vote and Comment on Facebook:Recommend This Page:
Post on Facebook Add to your del.icio.us Digg this story StumbleUpon Twitter Google Plus Post on Tumblr Add to Reddit Pin this story Linkedin Google Bookmark Blogger
Insert Your Personal Insight:

Please do not make mean comments and follow the biblical and spiritual character of this forum. If, however unpleasant situations arise, we request to flag it to us in order to evaluate the situation.

Text source: This text is in the public domain, downloaded from http://www.unboundbible.org, compiled by biblephone2008@gmail.com.

This project is based on delivering free-of-charge the Word of the Lord in all the world by using electronic means. If you want to contact us, you can do this by writing to the following e-mail: bible-study.xyz@hotmail.com


SELECT VERSION

COMPARE WITH OTHER BIBLES