Bible Study: FrontPage




 

Mithali, Chapter 7

Bible Study - Mithali 7 - Swahili - Swahili Union Bible - Web
 
 
 
Comment!       Comment Disqus!
  
1. Mwanangu, yashike maneno yangu, Na kuziweka amri zangu akiba kwako.
  
2. Uzishike amri zangu ukaishi, Na sheria yangu kama mboni ya jicho lako.
  
3. Zifunge katika vidole vyako; Ziandike juu ya kibao cha moyo wako.
  
4. Mwambie hekima, Wewe ndiwe umbu langu; Mwite ufahamu jamaa yako mwanamke.
  
5. Wapate kukulinda na malaya, Na mgeni akubembelezaye kwa maneno yake.
  
6. Maana katika dirisha la nyumba yangu Nalichungulia katika shubaka yake;
  
7. Nikaona katikati ya wajinga, Nikamtambua miongoni mwa vijana, Kijana mmoja asiyekuwa na akili,
  
8. Akipita njiani karibu na pembe yake, Akiishika njia iendayo nyumbani kwake,
  
9. Wakati wa magharibi, wakati wa jioni, Usiku wa manane, gizani.
  
10. Na tazama, mwanamke akamkuta, Ana mavazi ya kikahaba, mwerevu wa moyo;
  
11. Ana kelele, na ukaidi; Miguu yake haikai nyumbani mwake.
  
12. Mara yu katika njia kuu, mara viwanjani, Naye huotea kwenye pembe za kila njia.
  
13. Basi akamshika, akambusu, Akamwambia kwa uso usio na haya,
  
14. Kwangu ziko sadaka za amani; Leo hivi nimeziondoa nadhiri zangu;
  
15. Ndiyo maana nikatoka nikulaki, Nikutafute uso wako kwa bidii, nami nimekuona.
  
16. Nimetandika kitanda changu, magodoro mazuri, Kwa matandiko ya Kimisri yenye mistari.
  
17. Nimetia kitanda changu manukato, Manemane na udi na mdalasini.
  
18. Haya, na tushibe upendo hata asubuhi, Tujifurahishe nafsi zetu kwa mahaba.
  
19. Maana mume wangu hayumo nyumbani, Amekwenda safari ya mbali;
  
20. Amechukua mfuko wa fedha mkononi; Atarudi wakati wa mwezi mpevu.
  
21. Kwa maneno yake mengi na ulaini akamshawishi, Kwa ubembelezi wa midomo yake akamshinda.
  
22. Huyo akafuatana naye mara hiyo, Kama vile ng'ombe aendavyo machinjoni; Au mpumbavu kuadhibiwa katika pingu;
  
23. Hata mshale umchome maini; Kama ndege aendaye haraka mtegoni; Wala hajui ya kuwa ni hasara ya nafsi yake.
  
24. Basi, wanangu, nisikilizeni sasa, Mkayaangalie maneno ya kinywa changu.
  
25. Moyo wako usizielekee njia zake, Wala usipotee katika mapito yake.
  
26. Maana amewaangusha wengi waliojeruhi, Naam, jumla ya waliouawa naye ni jeshi kubwa.
  
27. Nyumba yake ni njia ya kwenda kuzimu, Hushuka mpaka vyumba vya mauti.


Search in:
Terms:

Vote and Comment on Facebook:Recommend This Page:
Post on Facebook Add to your del.icio.us Digg this story StumbleUpon Twitter Google Plus Post on Tumblr Add to Reddit Pin this story Linkedin Google Bookmark Blogger
Insert Your Personal Insight:

Please do not make mean comments and follow the biblical and spiritual character of this forum. If, however unpleasant situations arise, we request to flag it to us in order to evaluate the situation.

Text source: This text is in the public domain, downloaded from http://www.unboundbible.org, compiled by biblephone2008@gmail.com.

This project is based on delivering free-of-charge the Word of the Lord in all the world by using electronic means. If you want to contact us, you can do this by writing to the following e-mail: bible-study.xyz@hotmail.com


SELECT VERSION

COMPARE WITH OTHER BIBLES