Bible Study: FrontPage




 

Zaburi, Chapter 116

Bible Study - Zaburi 116 - Swahili - Swahili Union Bible - Web
 
 
 
Comment!       Comment Disqus!
  
1. Haleluya. Nampenda Bwana kwa kuwa anaisikiliza Sauti yangu na dua zangu.
  
2. Kwa maana amenitegea sikio lake, Kwa hiyo nitamwita siku zangu zote.
  
3. Kamba za mauti zilinizunguka, Shida za kuzimu zilinipata. Naliona taabu na huzuni;
  
4. Nikaliitia jina la Bwana. Ee Bwana, nakuomba sana, Uniokoe nafsi yangu.
  
5. Bwana ni mwenye neema na haki, Naam, Mungu wetu ni mwenye rehema.
  
6. Bwana huwalinda wasio na hila; Nalidhilika, akaniokoa.
  
7. Ee nafsi yangu, urudi rahani mwako, Kwa kuwa Bwana amekutendea ukarimu.
  
8. Maana umeniponya nafsi yangu na mauti, Macho yangu na machozi, Na miguu yangu na kuanguka.
  
9. Nitaenenda mbele za Bwana Katika nchi za walio hai.
  
10. Naliamini, kwa maana nitasema, Mimi naliteswa sana.
  
11. Mimi nalisema kwa haraka yangu, Wanadamu wote ni waongo.
  
12. Nimrudishie Bwana nini Kwa ukarimu wake wote alionitendea?
  
13. Nitakipokea kikombe cha wokovu; Na kulitangaza jina la Bwana;
  
14. Nitaziondoa nadhiri zangu kwa Bwana, Naam, mbele ya watu wake wote.
  
15. Ina thamani machoni pa Bwana Mauti ya wacha Mungu wake.
  
16. Ee Bwana, hakika mimi ni mtumishi wako, Mtumishi wako, mwana wa mjakazi wako, Umevifungua vifungo vyangu.
  
17. Nitakutolea dhabihu ya kushukuru; Na kulitangaza jina la Bwana;
  
18. Nitaziondoa nadhiri zangu kwa Bwana, Naam, mbele ya watu wake wote.
  
19. Katika nyua za nyumba ya Bwana, Ndani yako, Ee Yerusalemu.


Search in:
Terms:

Vote and Comment on Facebook:Recommend This Page:
Post on Facebook Add to your del.icio.us Digg this story StumbleUpon Twitter Google Plus Post on Tumblr Add to Reddit Pin this story Linkedin Google Bookmark Blogger
Insert Your Personal Insight:

Please do not make mean comments and follow the biblical and spiritual character of this forum. If, however unpleasant situations arise, we request to flag it to us in order to evaluate the situation.

Text source: This text is in the public domain, downloaded from http://www.unboundbible.org, compiled by biblephone2008@gmail.com.

This project is based on delivering free-of-charge the Word of the Lord in all the world by using electronic means. If you want to contact us, you can do this by writing to the following e-mail: bible-study.xyz@hotmail.com


SELECT VERSION

COMPARE WITH OTHER BIBLES