Bible Study: FrontPage




 

Zaburi, Chapter 144

Bible Study - Zaburi 144 - Swahili - Swahili Union Bible - Web
 
 
 
Comment!       Comment Disqus!
  
1. Na ahimidiwe Bwana, mwamba wangu, Anifundishaye mikono yangu vita, Vidole vyangu kupigana.
  
2. Mhisani wangu na boma langu, Ngome yangu na mwokozi wangu, Ngao yangu niliyemkimbilia, Huwatiisha watu wangu chini yangu.
  
3. Ee Bwana, mtu ni kitu gani hata umjue? Na binadamu hata umwangalie?
  
4. Binadamu amefanana na ubatili, Siku zake ni kama kivuli kipitacho.
  
5. Bwana, uziinamishe mbingu zako, ushuke, Uiguse milima nayo itatoka moshi.
  
6. Utupe umeme, uwatawanye, Uipige mishale yako, uwafadhaishe.
  
7. Uinyoshe mikono yako toka juu, uniponye, Unitoe katika maji mengi, katika mkono wa wageni.
  
8. Vinywa vyao vyasema visivyofaa, Na mkono wao wa kuume ni mkono wa uongo.
  
9. Ee Mungu, nitakuimbia wimbo mpya, Kwa kinanda chenye nyuzi kumi nitakuimbia.
  
10. Awapaye wafalme wokovu, Amwokoa Daudi, mtumishi wake, na upanga wa uovu.
  
11. Uniponye, unitoe, Katika mkono wa wageni. Vinywa vyao vyasema visivyofaa, Na mkono wao wa kuume ni mkono wa uongo.
  
12. Wana wetu na wawe kama miche Waliokua ujanani. Binti zetu kama nguzo za pembeni Zilizonakishwa kwa kupamba hekalu.
  
13. Ghala zetu na zijae Zenye akiba za jinsi zote. Kondoo zetu na wazae Elfu na makumi elfu mashambani mwetu.
  
14. Ng'ombe zetu na wachukue mizigo, Kusiwe na kushambuliwa. Wala kusiwe na kuhamishwa, Wala malalamiko katika njia zetu.
  
15. Heri watu wenye hali hiyo, Heri watu wenye Bwana kuwa Mungu wao.


Search in:
Terms:

Vote and Comment on Facebook:Recommend This Page:
Post on Facebook Add to your del.icio.us Digg this story StumbleUpon Twitter Google Plus Post on Tumblr Add to Reddit Pin this story Linkedin Google Bookmark Blogger
Insert Your Personal Insight:

Please do not make mean comments and follow the biblical and spiritual character of this forum. If, however unpleasant situations arise, we request to flag it to us in order to evaluate the situation.

Text source: This text is in the public domain, downloaded from http://www.unboundbible.org, compiled by biblephone2008@gmail.com.

This project is based on delivering free-of-charge the Word of the Lord in all the world by using electronic means. If you want to contact us, you can do this by writing to the following e-mail: bible-study.xyz@hotmail.com


SELECT VERSION

COMPARE WITH OTHER BIBLES