Bible Study: FrontPage




 

Zaburi, Chapter 29

Bible Study - Zaburi 29 - Swahili - Swahili Union Bible - Web
 
 
 
Comment!       Comment Disqus!
  
1. Mpeni Bwana, enyi wana wa Mungu, Mpeni Bwana utukufu na nguvu;
  
2. Mpeni Bwana utukufu wa jina lake; Mwabuduni Bwana kwa uzuri wa utakatifu.
  
3. Sauti ya Bwana i juu ya maji; Mungu wa utukufu alipiga radi; Bwana yu juu ya maji mengi.
  
4. Sauti ya Bwana ina nguvu; Sauti ya Bwana ina adhama;
  
5. Sauti ya Bwana yaivunja mierezi; Naam, Bwana aivunja-vunja mierezi ya Lebanoni;
  
6. Airusha-rusha kama ndama wa ng'ombe; Lebanoni na Sirioni kama mwana-nyati.
  
7. Sauti ya Bwana yaipasua miali ya moto;
  
8. Sauti ya Bwana yalitetemesha jangwa; Bwana alitetemesha jangwa la Kadeshi.
  
9. Sauti ya Bwana yawazalisha ayala, Na kuifichua misitu; Na ndani ya hekalu lake Wanasema wote, Utukufu.
  
10. Bwana aliketi juu ya Gharika; Naam, Bwana ameketi hali ya mfalme milele.
  
11. Bwana atawapa watu wake nguvu; Bwana atawabariki watu wake kwa amani.


Search in:
Terms:

Vote and Comment on Facebook:Recommend This Page:
Post on Facebook Add to your del.icio.us Digg this story StumbleUpon Twitter Google Plus Post on Tumblr Add to Reddit Pin this story Linkedin Google Bookmark Blogger
Insert Your Personal Insight:

Please do not make mean comments and follow the biblical and spiritual character of this forum. If, however unpleasant situations arise, we request to flag it to us in order to evaluate the situation.

Text source: This text is in the public domain, downloaded from http://www.unboundbible.org, compiled by biblephone2008@gmail.com.

This project is based on delivering free-of-charge the Word of the Lord in all the world by using electronic means. If you want to contact us, you can do this by writing to the following e-mail: bible-study.xyz@hotmail.com


SELECT VERSION

COMPARE WITH OTHER BIBLES