Bible Study: FrontPage




 

Zaburi, Chapter 38

Bible Study - Zaburi 38 - Swahili - Swahili Union Bible - Web
 
 
 
Comment!       Comment Disqus!
  
1. Ee Bwana, usinilaumu katika ghadhabu yako, Wala usiniadhibu kwa ukali wa hasira yako.
  
2. Kwa maana mishale yako imenichoma, Na mkono wako umenipata.
  
3. Hamna uzima katika mwili wangu Kwa sababu ya ghadhabu yako. Wala hamna amani mifupani mwangu Kwa sababu ya hatia zangu.
  
4. Maana dhambi zangu zimenifunikiza kichwa, Kama mzigo mzito zimenilemea mno.
  
5. Jeraha zangu zinanuka, zimeoza, Kwa sababu ya upumbavu wangu.
  
6. Nimepindika na kuinama sana, Mchana kutwa nimekwenda nikihuzunika.
  
7. Maana viuno vyangu vimejaa homa, Wala hamna uzima katika mwili wangu.
  
8. Nimedhoofika na kuchubuka sana, Nimeugua kwa fadhaa ya moyo wangu.
  
9. Bwana, haja zangu zote ziko mbele zako, Kuugua kwangu hakukusitirika kwako.
  
10. Moyo wangu unapwita-pwita, Nguvu zangu zimeniacha; Nuru ya macho yangu nayo imeniondoka.
  
11. Wanipendao na rafiki zangu wanasimama mbali na pigo langu; Naam, karibu zangu wamesimama mbali.
  
12. Nao wanaoutafuta uhai wangu hutega mitego; Nao wanaotaka kunidhuru hunena mabaya; Na kufikiri hila mchana kutwa.
  
13. Lakini kama kiziwi sisikii, Nami ni kama bubu asiyefumbua kinywa chake.
  
14. Naam, nimekuwa kama mtu asiyesikia, Ambaye hamna hoja kinywani mwake.
  
15. Kwa kuwa nakungoja Wewe, Bwana, Wewe utajibu, Ee Bwana, Mungu wangu.
  
16. Maana nalisema, Wasije wakanifurahia; Mguu wangu ukiteleza wajitukuza juu yangu.
  
17. Kwa maana mimi ni karibu na kusita, Na maumivu yangu yako mbele yangu daima.
  
18. Kwa maana nitaungama uovu wangu, Na kusikitika kwa dhambi zangu.
  
19. Lakini adui zangu ni wazima wenye nguvu, Nao wanaonichukia bure wamekuwa wengi.
  
20. Naam, wakilipa mabaya kwa mema, Huwa adui zangu kwa kuwa nalifuata lililo jema.
  
21. Wewe, Bwana, usiniache, Mungu wangu, usijitenge nami.
  
22. Ufanye haraka kunisaidia, Ee Bwana, wokovu wangu.


Search in:
Terms:

Vote and Comment on Facebook:Recommend This Page:
Post on Facebook Add to your del.icio.us Digg this story StumbleUpon Twitter Google Plus Post on Tumblr Add to Reddit Pin this story Linkedin Google Bookmark Blogger
Insert Your Personal Insight:

Please do not make mean comments and follow the biblical and spiritual character of this forum. If, however unpleasant situations arise, we request to flag it to us in order to evaluate the situation.

Text source: This text is in the public domain, downloaded from http://www.unboundbible.org, compiled by biblephone2008@gmail.com.

This project is based on delivering free-of-charge the Word of the Lord in all the world by using electronic means. If you want to contact us, you can do this by writing to the following e-mail: bible-study.xyz@hotmail.com


SELECT VERSION

COMPARE WITH OTHER BIBLES