|
|
Zaburi, Chapter 60
1. Ee Mungu, umetutupa na kututawanya, Umekuwa na hasira, uturudishe tena.
2. Umeitetemesha nchi na kuipasua, Upaponye palipobomoka, maana inatikisika.
3. Umewaonyesha watu wako mazito, Na kutunywesha mvinyo ya kutuyumbisha.
4. Umewapa wakuogopao bendera, Ili itwekwe kwa ajili ya kweli.
5. Ili wapenzi wako waopolewe, Uokoe kwa mkono wako wa kuume, utuitikie.
6. Mungu amenena kwa utakatifu wake, Nami nitashangilia. Nitaigawanya Shekemu, Nitalipima bonde la Sukothi.
7. Gileadi ni yangu, na Manase ni yangu, Na Efraimu ni nguvu ya kichwa changu. Yuda ni fimbo yangu ya kifalme,
8. Moabu ni bakuli langu la kunawia. Nitamtupia Edomu kiatu changu, Na kumpigia Filisti kelele za vita.
9. Ni nani atakayenipeleka hata mji wenye boma? Ni nani atakayeniongoza hata Edomu?
10. Ee Mungu, si Wewe uliyetutupa? Wala, Ee Mungu, hutoki na majeshi yetu?
11. Utuletee msaada juu ya mtesi, Maana wokovu wa binadamu haufai.
12. Kwa msaada wa Mungu tutatenda makuu, Maana Yeye atawakanyaga watesi wetu.
|
|
Text source: This text is in the public domain, downloaded from http://www.unboundbible.org, compiled by biblephone2008@gmail.com.
|
| |
| This project is based on delivering free-of-charge the Word of the Lord in all the world by using electronic means. If you want to contact us, you can do this by writing to the following e-mail: bible-study.xyz@hotmail.com |
|
|
|
SELECT VERSION
COMPARE WITH OTHER BIBLES
|
|