Bible Study: FrontPage




 

Zaburi, Chapter 69

Bible Study - Zaburi 69 - Swahili - Swahili Union Bible - Web
 
 
 
Comment!       Comment Disqus!
  
1. Ee Mungu, uniokoe, Maana maji yamefika mpaka nafsini mwangu.
  
2. Ninazama katika matope mengi, Pasipowezekana kusimama. Nimefika penye maji ya vilindi, Mkondo wa maji unanigharikisha.
  
3. Nimechoka kwa kulia kwangu, Koo yangu imekauka. Macho yangu yamedhoofu Kwa kumngoja Mungu wangu.
  
4. Wanaonichukia bure ni wengi Kuliko nywele za kichwa changu. Watakao kunikatilia mbali wamekuwa hodari, Adui zangu kwa sababu isiyo kweli. Hata mimi nalilipishwa kwa nguvu Vitu nisivyovichukua.
  
5. Ee Mungu, unajua upumbavu wangu, Wala hukufichwa dhambi yangu.
  
6. Wanaokungoja Wewe wasiaibishwe, Kwa ajili yangu, Bwana, MUNGU wa majeshi. Wanaokutafuta Wewe wasifedheheshwe, Kwa ajili yangu, Ee Mungu wa Israeli.
  
7. Maana kwa ajili yako nimestahimili laumu, Fedheha imenifunika uso wangu.
  
8. Nimekuwa mgeni kwa ndugu zangu, Na msikwao kwa wana wa mama yangu.
  
9. Maana wivu wa nyumba yako umenila, Na laumu zao wanaokulaumu zimenipata.
  
10. Nilipolia na kuiadhibu roho yangu kwa kufunga, Ikawa laumu juu yangu.
  
11. Nilipofanya gunia kuwa nguo zangu, Nikawa mithali kwao.
  
12. Waketio langoni hunisema, Na nyimbo za walevi hunidhihaki.
  
13. Nami maombi yangu nakuomba Wewe, Bwana, Wakati ukupendezao; Ee Mungu, Kwa wingi wa fadhili zako unijibu, Katika kweli ya wokovu wako.
  
14. Uniponye kwa kunitoa matopeni, Wala usiniache nikazama. Na niponywe nao wanaonichukia, Na katika vilindi vya maji.
  
15. Mkondo usinigharikishe, wala vilindi visinimeze, Wala shimo lisifumbe kinywa chake juu yangu.
  
16. Ee Bwana, unijibu, maana fadhili zako ni njema, Kwa kadiri ya rehema zako unielekee.
  
17. Wala usinifiche uso wako, mimi mtumishi wako, Maana mimi nimo taabuni, unijibu upesi.
  
18. Uikaribie nafsi yangu, uikomboe, Kwa sababu ya adui zangu unifidie.
  
19. Wewe umejua kulaumiwa kwangu, Na kuaibika na kufedheheka kwangu, Mbele zako Wewe wako watesi wangu wote.
  
20. Laumu imenivunja moyo, Nami ninaugua sana. Nikangoja aje wa kunihurumia, wala hakuna; Na wa kunifariji, wala sikumwona mtu.
  
21. Wakanipa uchungu kuwa chakula changu; Nami nilipokuwa na kiu wakaninywesha siki.
  
22. Meza yao mbele yao na iwe mtego; Naam, wakiwa salama na iwe tanzi.
  
23. Macho yao yatiwe giza wasione, Na viuno vyao uvitetemeshe daima.
  
24. Uimwage ghadhabu yako juu yao, Na ukali wa hasira yako uwapate.
  
25. Matuo yao na yawe ukiwa, Pasiwe na mtu wa kukaa hemani mwao.
  
26. Maana wanamwudhi mtu uliyempiga Wewe, Wanasimulia maumivu ya hao uliowatia jeraha.
  
27. Uwaongezee uovu juu ya uovu, Wala wasiingie katika haki yako.
  
28. Na wafutwe katika chuo cha uhai, Wala pamoja na wenye haki wasiandikwe.
  
29. Nami niliye maskini na mtu wa huzuni, Mungu, wokovu wako utaniinua.
  
30. Nitalisifu jina la Mungu kwa wimbo, Nami nitamtukuza kwa shukrani.
  
31. Nayo yatampendeza Bwana kuliko ng'ombe, Au ndama mwenye pembe na kwato.
  
32. Walioonewa watakapoona watafurahi; Enyi mmtafutao Mungu, mioyo yenu ihuishwe.
  
33. Kwa kuwa Bwana huwasikia wahitaji, Wala hawadharau wafungwa wake.
  
34. Mbingu na nchi zimsifu, Bahari na vyote viendavyo ndani yake.
  
35. Maana Mungu ataiokoa Sayuni, na kuijenga miji ya Yuda, Na watu watakaa ndani yake na kuimiliki.
  
36. Wazao wa watumishi wake watairithi, Nao walipendao jina lake watakaa humo.


Search in:
Terms:

Vote and Comment on Facebook:Recommend This Page:
Post on Facebook Add to your del.icio.us Digg this story StumbleUpon Twitter Google Plus Post on Tumblr Add to Reddit Pin this story Linkedin Google Bookmark Blogger
Insert Your Personal Insight:

Please do not make mean comments and follow the biblical and spiritual character of this forum. If, however unpleasant situations arise, we request to flag it to us in order to evaluate the situation.

Text source: This text is in the public domain, downloaded from http://www.unboundbible.org, compiled by biblephone2008@gmail.com.

This project is based on delivering free-of-charge the Word of the Lord in all the world by using electronic means. If you want to contact us, you can do this by writing to the following e-mail: bible-study.xyz@hotmail.com


SELECT VERSION

COMPARE WITH OTHER BIBLES