|
|
Zaburi, Chapter 75
1. Ee Mungu, twakushukuru. Twakushukuru kwa kuwa Jina lako li karibu; Watu huyasimulia matendo yako ya ajabu.
2. Nitakapoufikia wakati ulioamriwa, Mimi nitahukumu hukumu za haki.
3. Ingawa dunia na wote wakaao humo wataharuki, Mimi mwenyewe nimezisimamisha nguzo zake.
4. Naliwaambia waliojivuna, Msijivune; Na wasio haki, Msiiinue pembe.
5. Msiiinue pembe yenu juu, Wala msinene kwa shingo ya kiburi.
6. Maana siko mashariki wala magharibi, Wala nyikani itokako heshima.
7. Bali Mungu ndiye ahukumuye; Humdhili huyu na kumwinua huyu.
8. Maana mkononi mwa Bwana mna kikombe, Na mvinyo yake inatoka povu; Kumejaa machanganyiko; Naye huyamimina. Na sira zake wasio haki wa dunia Watazifyonza na kuzinywa.
9. Bali mimi nitatangaza matendo yako milele, Nitamwimbia Mungu wa Yakobo.
10. Pembe zote za wasio haki nitazikata, Na pembe za mwenye haki zitainuka.
|
|
Text source: This text is in the public domain, downloaded from http://www.unboundbible.org, compiled by biblephone2008@gmail.com.
|
| |
| This project is based on delivering free-of-charge the Word of the Lord in all the world by using electronic means. If you want to contact us, you can do this by writing to the following e-mail: bible-study.xyz@hotmail.com |
|
|
|
SELECT VERSION
COMPARE WITH OTHER BIBLES
|
|