Bible Study: FrontPage




 

Zaburi, Chapter 77

Bible Study - Zaburi 77 - Swahili - Swahili Union Bible - Web
 
 
 
Comment!       Comment Disqus!
  
1. Nimpazie Mungu sauti yangu, Naam, nimpazie Mungu, naye atanisikia.
  
2. Siku ya taabu yangu nalimtafuta Bwana; Mkono wangu ulinyoshwa usiku, haukulegea; Nafsi yangu ilikataa kufarijika.
  
3. Nilipotaka kumkumbuka Mungu nalifadhaika; Nilipotaka kutafakari roho yangu ilizimia.
  
4. Ulizishika kope za macho yangu zisifumbike; Naliona mashaka nisiweze kunena.
  
5. Nalifikiri habari za siku za kale, Miaka ya zamani zilizopita.
  
6. Nakumbuka wimbo wangu usiku, Nawaza moyoni mwangu, Roho yangu ikatafuta.
  
7. Je! Bwana atatupa milele na milele? Hatatenda fadhili tena kabisa?
  
8. Rehema zake zimekoma hata milele? Ahadi yake imekwisha hata vizazi vyote?
  
9. Mungu amesahau fadhili zake? Amezuia kwa hasira rehema zake?
  
10. Nikasema, Ndio udhaifu wangu huo; Lakini nitaikumbuka miaka ya mkono wa kuume wake Aliye juu.
  
11. Nitayakumbuka matendo ya Bwana; Naam, nitayakumbuka maajabu yako ya kale.
  
12. Pia nitaitafakari kazi yako yote; Nitaziwaza habari za matendo yako.
  
13. Ee Mungu, njia yako i katika utakatifu; Ni nani aliye mungu mkuu kama Mungu?
  
14. Wewe ndiwe Mungu ufanyaye maajabu; Uliudhihirisha uweza wako kati ya mataifa.
  
15. Kwa mkono wako umewakomboa watu wako, Wana wa Yakobo na Yusufu.
  
16. Ee Mungu, yale maji yalikuona, Yale maji yalikuona, yakaogopa. Vilindi vya maji navyo vikatetemeka,
  
17. Mawingu yakamwaga maji. Mbingu nazo zikatoa sauti, Mishale yako nayo ikatapakaa.
  
18. Sauti ya radi yako ikawa katika kisulisuli; Umeme uliuangaza ulimwengu. Nchi ilitetemeka na kutikisika;
  
19. Njia yako ilikuwa katika bahari. Na mapito yako yalikuwa katika maji makuu; Hatua zako hazikujulikana.
  
20. Uliwaongoza watu wako kama kundi, Kwa mkono wa Musa na Haruni.


Search in:
Terms:

Vote and Comment on Facebook:Recommend This Page:
Post on Facebook Add to your del.icio.us Digg this story StumbleUpon Twitter Google Plus Post on Tumblr Add to Reddit Pin this story Linkedin Google Bookmark Blogger
Insert Your Personal Insight:

Please do not make mean comments and follow the biblical and spiritual character of this forum. If, however unpleasant situations arise, we request to flag it to us in order to evaluate the situation.

Text source: This text is in the public domain, downloaded from http://www.unboundbible.org, compiled by biblephone2008@gmail.com.

This project is based on delivering free-of-charge the Word of the Lord in all the world by using electronic means. If you want to contact us, you can do this by writing to the following e-mail: bible-study.xyz@hotmail.com


SELECT VERSION

COMPARE WITH OTHER BIBLES