Bible Study: FrontPage




 

Zaburi, Chapter 88

Bible Study - Zaburi 88 - Swahili - Swahili Union Bible - Web
 
 
 
Comment!       Comment Disqus!
  
1. Ee Bwana, Mungu wa wokovu wangu Mchana na usiku nimelia mbele zako.
  
2. Maombi yangu yafike mbele zako, Uutegee ukelele wangu sikio lako.
  
3. Maana nafsi yangu imeshiba taabu, Na uhai wangu umekaribia kuzimu.
  
4. Nimehesabiwa pamoja nao washukao shimoni; Nimekuwa kama mtu asiye na msaada.
  
5. Miongoni mwao waliokufa nimetupwa, Kama waliouawa walalao makaburini. Hao ambao Wewe huwakumbuki tena, Wametengwa mbali na mkono wako.
  
6. Mimi umenilaza katika shimo la chini, Katika mahali penye giza vilindini.
  
7. Ghadhabu yako imenilemea, Umenitesa kwa mawimbi yako yote.
  
8. Wanijuao umewatenga nami; Umenifanya kuwa chukizo kwao; Nimefungwa wala siwezi kutoka.
  
9. Jicho langu limefifia kwa ajili ya mateso Bwana, nimekuita kila siku; Nimekunyoshea Wewe mikono yangu.
  
10. Wafu je! Utawafanyia miujiza? Au waliofariki watasimama na kukuhimidi?
  
11. Fadhili zako zitasimuliwa kaburini? Au uaminifu wako katika uharibifu?
  
12. Miujiza yako itajulikana gizani? Au haki yako katika nchi ya usahaulifu?
  
13. Lakini mimi nimekulilia Wewe, Bwana, Na asubuhi maombi yangu yatakuwasilia.
  
14. Bwana, kwa nini kuitupa nafsi yangu, Na kunificha uso wako?
  
15. Nateswa mimi hali ya kufa tangu ujana, Nimevumilia vitisho vyako na kufadhaika.
  
16. Hasira zako kali zimepita juu yangu, Maogofyo yako yameniangamiza.
  
17. Yamenizunguka kama maji mchana kutwa, Yamenisonga yote pamoja.
  
18. Mpenzi na rafiki umewatenga nami, Nao wanijuao wamo gizani.


Search in:
Terms:

Vote and Comment on Facebook:Recommend This Page:
Post on Facebook Add to your del.icio.us Digg this story StumbleUpon Twitter Google Plus Post on Tumblr Add to Reddit Pin this story Linkedin Google Bookmark Blogger
Insert Your Personal Insight:

Please do not make mean comments and follow the biblical and spiritual character of this forum. If, however unpleasant situations arise, we request to flag it to us in order to evaluate the situation.

Text source: This text is in the public domain, downloaded from http://www.unboundbible.org, compiled by biblephone2008@gmail.com.

This project is based on delivering free-of-charge the Word of the Lord in all the world by using electronic means. If you want to contact us, you can do this by writing to the following e-mail: bible-study.xyz@hotmail.com


SELECT VERSION

COMPARE WITH OTHER BIBLES