Bible Study: FrontPage




 

Zaburi, Chapter 94

Bible Study - Zaburi 94 - Swahili - Swahili Union Bible - Web
 
 
 
Comment!       Comment Disqus!
  
1. Ee Bwana, Mungu wa kisasi, Mungu wa kisasi, uangaze,
  
2. Mwenye kuihukumu nchi, ujitukuze, Uwape wenye kiburi stahili zao.
  
3. Bwana, hata lini wasio haki, Hata lini wasio haki watashangilia?
  
4. Je! Wote watendao uovu watatoa maneno, Na kusema majivuno, na kufanya kiburi?
  
5. Ee Bwana, wanawaseta watu wako; Wanautesa urithi wako;
  
6. Wanamwua mjane na mgeni; Wanawafisha yatima.
  
7. Nao husema, Bwana haoni; Mungu wa Yakobo hafikiri.
  
8. Enyi wajinga miongoni mwa watu, fikirini; Enyi wapumbavu, lini mtakapopata akili?
  
9. Aliyelitia sikio mahali pake asisikie? Aliyelifanya jicho asione?
  
10. Awaadibuye mataifa asikemee? Amfundishaye mwanadamu asijue?
  
11. Bwana anajua mawazo ya mwanadamu, Ya kuwa ni ubatili.
  
12. Ee Bwana, heri mtu yule umwadibuye, Na kumfundisha kwa sheria yako;
  
13. Upate kumstarehesha siku za mabaya, Hata asiye haki atakapochimbiwa shimo.
  
14. Kwa kuwa Bwana hatawatupa watu wake, Wala hutauacha urithi wake,
  
15. Maana hukumu itairejea haki, Na wote walio wanyofu wa moyo wataifuata.
  
16. Ni nani atakayesimama Kwa ajili yangu juu ya wabaya? Ni nani atakayenisaidia Juu yao wafanyao maovu?
  
17. Kama Bwana asingalikuwa msaada wangu, Nafsi yangu kwa upesi ingalikaa penye kimya.
  
18. Niliposema, Mguu wangu unateleza; Ee Bwana, fadhili zako zilinitegemeza.
  
19. Katika wingi wa mawazo ya moyoni mwangu, Faraja zako zaifurahisha roho yangu.
  
20. Je! Kiti cha udhalimu kishirikiane nawe, Kitungacho madhara kwa njia ya sheria?
  
21. Huishambulia nafsi yake mwenye haki, Na kuihukumu damu isiyo na hatia.
  
22. Lakini Bwana amekuwa ngome kwangu, Na Mungu wangu mwamba wangu wa kukimbilia.
  
23. Naye atawarudishia uovu wao, Atawaangamiza katika ubaya wao, Naam, Bwana, Mungu wetu, atawaangamiza.


Search in:
Terms:

Vote and Comment on Facebook:Recommend This Page:
Post on Facebook Add to your del.icio.us Digg this story StumbleUpon Twitter Google Plus Post on Tumblr Add to Reddit Pin this story Linkedin Google Bookmark Blogger
Insert Your Personal Insight:

Please do not make mean comments and follow the biblical and spiritual character of this forum. If, however unpleasant situations arise, we request to flag it to us in order to evaluate the situation.

Text source: This text is in the public domain, downloaded from http://www.unboundbible.org, compiled by biblephone2008@gmail.com.

This project is based on delivering free-of-charge the Word of the Lord in all the world by using electronic means. If you want to contact us, you can do this by writing to the following e-mail: bible-study.xyz@hotmail.com


SELECT VERSION

COMPARE WITH OTHER BIBLES