|
|
Zaburi, Chapter 98
1. Mwimbieni Bwana wimbo mpya, Kwa maana ametenda mambo ya ajabu. Mkono wa kuume wake mwenyewe, Mkono wake mtakatifu umemtendea wokovu.
2. Bwana ameufunua wokovu wake, Machoni pa mataifa ameidhihirisha haki yake.
3. Amezikumbuka rehema zake, Na uaminifu wake kwa nyumba ya Israeli. Miisho yote ya dunia imeuona Wokovu wa Mungu wetu.
4. Mshangilieni Bwana, nchi yote, Inueni sauti, imbeni kwa furaha, imbeni zaburi.
5. Mwimbieni Bwana zaburi kwa kinubi, Kwa kinubi na sauti ya zaburi.
6. Kwa panda na sauti ya baragumu. Shangilieni mbele za Mfalme, Bwana.
7. Bahari na ivume na vyote viijazavyo, Ulimwengu nao wanaokaa ndani yake.
8. Mito na ipige makofi, Milima na iimbe pamoja kwa furaha.
9. Mbele za Bwana; Kwa maana anakuja aihukumu nchi. Atauhukumu ulimwengu kwa haki, Na mataifa kwa adili.
|
|
Text source: This text is in the public domain, downloaded from http://www.unboundbible.org, compiled by biblephone2008@gmail.com.
|
| |
| This project is based on delivering free-of-charge the Word of the Lord in all the world by using electronic means. If you want to contact us, you can do this by writing to the following e-mail: bible-study.xyz@hotmail.com |
|
|
|
SELECT VERSION
COMPARE WITH OTHER BIBLES
|
|