Bible Study: FrontPage




 

Mathayo, Chapter 17

Bible Study - Mathayo 17 - Swahili - Swahili New Testament - Web
 
 
 
Comment!       Comment Disqus!
  
1. Baada ya siku sita, Yesu aliwachukua Petro, Yakobo na Yohane nduguye, akaenda nao peke yao juu ya mlima mrefu.
  
2. Huko, wakiwa wanamtazama, akageuka sura, uso wake ukang`aa kama jua na mavazi yake yakawa meupe kama nuru.
  
3. Mose na Eliya wakawatokea, wakawa wanazungumza naye.
  
4. Hapo Petro akamwambia Yesu, "Bwana, ni vizuri sana kwamba tupo hapa! Ukipenda nitajenga vibanda vitatu: kimoja chako, kimoja cha Mose nakimoja cha Eliya."
  
5. Alipokuwa bado anasema hivyo, wingu jeupe likawafunika, na sauti ikasikika kutoka katika hilo wingu: "Huyu ni Mwanangu mpendwa,ninayependezwa naye, msikilizeni."
  
6. Wanafunzi waliposikia hivyo wakaanguka kifudifudi, wakaogopa sana.
  
7. Yesu akawaendea, akawagusa, akasema, "Simameni, msiogope!"
  
8. Walipoinua macho yao hawakumwona mtu, ila Yesu peke yake.
  
9. Basi, walipokuwa wanashuka mlimani, Yesu akawaonya: "Msimwambie mtu mambo mliyoyaona mpaka Mwana wa Mtu atakapofufuliwa kutoka wafu."
  
10. Kisha wanafunzi wakamwuliza, "Mbona walimu wa Sheria wanasema ati ni lazima kwanza Eliya aje?"
  
11. Yesu akawajibu, "Kweli, Eliya atakuja kutayarisha mambo yote.
  
12. Lakini nawaambieni, Eliya amekwisha kuja nao hawakumtambua, bali walimtendea jinsi walivyotaka. Mwana wa Mtu atateswa vivyo hivyomikononi mwao."
  
13. Hapo hao wanafunzi wakafahamu kwamba alikuwa akiwaambia juu ya Yohane mbatizaji.
  
14. Walipojiunga tena na ule umati wa watu, mtu mmoja alimwendea Yesu, akampigia magoti,
  
15. akasema, "Mheshimiwa, mwonee huruma mwanangu kwa kuwa ana kifafa, tena anateseka sana; mara nyingi yeye huanguka motoni na majini.
  
16. Nilimleta kwa wanafunzi wako lakini hawakuweza kumponya."
  
17. Yesu akajibu, "Enyi kizazi kisicho na imani, kilichopotoka! Nitakaa nanyi mpaka lini? Nitawavumilia ninyi mpaka lini? Mleteni hapa huyomtoto."
  
18. Basi, Yesu akamkemea huyo pepo, naye akamtoka, na yule mtoto akapona wakati huohuo.
  
19. Kisha wanafunzi wakamwendea Yesu kwa faragha, wakamwuliza, "Kwa nini sisi hatukuweza kumtoa yule pepo?"
  
20. Yesu akawajibu, "Kwa sababu ya imani yenu haba. Nawaambieni kweli, kama tu mkiwa na imani, hata iwe ndogo kama mbegu ya haradali, mtawezakuuambia mlima huu: `Toka hapa uende pale,` nao utakwenda. Hakunachochote ambacho hakingewezekana kwenu."*fg* kuondolewa ila kwa salana kufunga."
  
21. missing
  
22. Walipokuwa pamoja huko Galilaya, Yesu aliwaambia, "Mwana wa Mtu atakabidhiwa kwa watu.
  
23. Watamuua, lakini siku ya tatu atafufuliwa." Wanafunzi wakahuzunika mno.
  
24. Walipofika Kafarnaumu watu wenye kukusanya fedha ya zaka ya Hekalu walimwendea Petro, wakamwuliza, "Je, mwalimu wenu hulipa fedha yazaka?"
  
25. Petro akajibu, "Naam, hulipa." Basi, Petro alipoingia ndani ya nyumba, kabla hata hajasema neno, Yesu akamwuliza, "Simoni, weweunaonaje? Wafalme wa dunia hukusanya ushuru au kodi kutoka kwa kinanani? Kutoka kwa wananchi ama kutoka kwa wageni?"
  
26. Petro akajibu, "Kutoka kwa wageni." Yesu akamwambia, "Haya basi, wananchi hawahusiki.
  
27. Lakini kusudi tusiwakwaze, nenda ziwani ukatupe ndoana; chukua samaki wa kwanza atakayenaswa, fungua kinywa chake, na ndani utakutafedha taslimu ya zaka. Ichukue ukawape kwa ajili yangu na kwa ajiliyako."


Search in:
Terms:

Vote and Comment on Facebook:Recommend This Page:
Post on Facebook Add to your del.icio.us Digg this story StumbleUpon Twitter Google Plus Post on Tumblr Add to Reddit Pin this story Linkedin Google Bookmark Blogger
Insert Your Personal Insight:

Please do not make mean comments and follow the biblical and spiritual character of this forum. If, however unpleasant situations arise, we request to flag it to us in order to evaluate the situation.

Text source: Swahili New Testament, public domain.

This project is based on delivering free-of-charge the Word of the Lord in all the world by using electronic means. If you want to contact us, you can do this by writing to the following e-mail: bible-study.xyz@hotmail.com


SELECT VERSION

COMPARE WITH OTHER BIBLES