Bible Study: FrontPage




 

Mathayo, Chapter 18

Bible Study - Mathayo 18 - Swahili - Swahili New Testament - Web
 
 
 
Comment!       Comment Disqus!
  
1. Wakati ule wanafunzi walimwendea Yesu, wakamwuliza, "Ni nani aliye mkuu katika Ufalme wa mbinguni?"
  
2. Yesu akamwita mtoto mmoja, akamsimamisha kati yao,
  
3. kisha akasema, "Nawaambieni kweli, msipogeuka na kuwa kama watoto, hamtaingia kamwe katika Ufalme wa mbinguni.
  
4. Yeyote anayejinyenyekesha kama mtoto huyu, huyo ndiye aliye mkubwa katika Ufalme wa mbinguni.
  
5. Yeyote anayemkaribisha mtoto mmoja kama huyu kwa jina langu, ananikaribisha mimi.
  
6. "Yeyote atakayemkosesha mmoja wa hawa wadogo wanaoniamini, ingekuwa afadhali afungwe shingoni jiwe kubwa la kusagia na kuzamishwa kwenyekilindi cha bahari.
  
7. Ole wake ulimwengu kwa sababu ya vikwazo vinavyowaangusha wengine. Vikwazo hivyo ni lazima vitokee lakini ole wake mtu yuleatakayevisababisha.
  
8. "Kama mkono au mguu wako ukikukosesha, ukate na kuutupa mbali nawe. Ni afadhali kwako kuingia katika uzima bila mkono au mguu, kulikokutupwa katika moto wa milele ukiwa na mikono miwili na miguu yakomiwili.
  
9. Na kama jicho lako likikukosesha, ling`oe na kulitupa mbali nawe. Ni afadhali kwako kuingia katika uzima ukiwa chongo, kuliko kutupwakatika moto wa Jehanamu ukiwa na macho yako yote mawili.
  
10. "Jihadharini! Msimdharau mmojawapo wa wadogo hawa. Nawaambieni, malaika wao huko mbinguni wako daima mbele ya Baba yangu aliyembinguni.*fh*
  
11. missing
  
12. Mnaonaje? Mtu akiwa na kondoo mia, akimpoteza mmoja, hufanyaje? Huwaacha wale tisini na tisa mlimani, na huenda kumtafuta yulealiyepotea.
  
13. Akimpata, nawaambieni kweli, humfurahia huyo kuliko awafurahiavyo wale tisini na tisa ambao hawakupotea.
  
14. Hali kadhalika, Baba yenu wa mbinguni hapendi hata mmoja wa hawa wadogo apotee.
  
15. "Ndugu yako akikukosea, mwendee ukamwonye mkiwa ninyi peke yenu. Akikusikia utakuwa umempata ndugu yako.
  
16. Asipokusikia, chukua mtu mmoja au wawili pamoja nawe, ili kwa mawaidha ya mashahidi wawili au watatu, kila tatizo litatuliwe.
  
17. Asipowasikia hao, liambie kanisa. Na kama hatalisikia kanisa, na awe kwako kama watu wasiomjua Mungu na watoza ushuru.
  
18. "Nawaambieni kweli, mtakachofunga duniani kitafungwa mbinguni, na mtakachofungua duniani kitafunguliwa mbinguni.
  
19. Tena nawaambieni, wawili miongoni mwenu wakikubaliana hapa duniani kuhusu jambo lolote la kuomba, Baba yangu wa mbinguni atawafanyiajambo hilo.
  
20. Kwa maana popote pale wanapokusanyika wawili au watatu kwa jina langu, mimi nipo hapo kati yao."
  
21. Kisha Petro akamwendea Yesu, akamwuliza, "Je, ndugu yangu akinikosea, nimsamehe mara ngapi? Mara saba?"
  
22. Yesu akamjibu, "Sisemi mara saba tu, bali sabini mara saba.
  
23. Ndiyo maana Ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme mmoja aliyeamua kukagua hesabu za watumishi wake.
  
24. Ukaguzi ulipoanza, akaletewa mtu mmoja aliyekuwa na deni la fedha talanta elfu kumi.
  
25. Mtu huyo hakuwa na chochote cha kulipa; hivyo bwana wake aliamuru wauzwe, yeye, mke wake, watoto wake na vitu vyote alivyokuwa navyo,ili deni lilipwe.
  
26. Basi, huyo mtumishi akapiga magoti mbele yake, akasema, `Unisubiri nami nitakulipa deni lote.`
  
27. Yule bwana alimwonea huruma, akamsamehe lile deni, akamwacha aende zake.
  
28. "Lakini huyo mtumishi akaondoka, akamkuta mmoja wa watumishi wenzake aliyekuwa na deni lake fedha denari mia moja. Akamkamata, akamkaba kooakisema, `Lipa deni lako!`
  
29. Huyo mtumishi mwenzake akapiga magoti, akamwomba, `Unisubiri nami nitalipa deni langu lote.`
  
30. Lakini yeye hakutaka, bali alimtia gerezani mpaka hapo atakapolipa lile deni.
  
31. "Basi, watumishi wenzake walipoona jambo hilo walisikitika sana, wakaenda kumpasha habari bwana wao juu ya mambo hayo yaliyotukia.
  
32. Hapo yule bwana alimwita huyo mtumishi, akamwambia, `Wewe ni mtumishi mbaya sana! Uliniomba, nami nikakusamehe deni lako lote.
  
33. Je, haikukupasa nawe kumhurumia mtumishi mwenzako kama nilivyokuhurumia?`
  
34. "Basi, huyo bwana alikasirika sana, akamtoa huyo mtumishi aadhibiwe mpaka hapo atakapolipa deni lote.
  
35. Na baba yangu aliye mbinguni atawafanyieni vivyo hivyo kama kila mmoja wenu hatamsamehe ndugu yake kwa moyo wake wote."


Search in:
Terms:

Vote and Comment on Facebook:Recommend This Page:
Post on Facebook Add to your del.icio.us Digg this story StumbleUpon Twitter Google Plus Post on Tumblr Add to Reddit Pin this story Linkedin Google Bookmark Blogger
Insert Your Personal Insight:

Please do not make mean comments and follow the biblical and spiritual character of this forum. If, however unpleasant situations arise, we request to flag it to us in order to evaluate the situation.

Text source: Swahili New Testament, public domain.

This project is based on delivering free-of-charge the Word of the Lord in all the world by using electronic means. If you want to contact us, you can do this by writing to the following e-mail: bible-study.xyz@hotmail.com


SELECT VERSION

COMPARE WITH OTHER BIBLES