Bible Study: FrontPage




 

Mathayo, Chapter 3

Bible Study - Mathayo 3 - Swahili - Swahili New Testament - Web
 
 
 
Comment!       Comment Disqus!
  
1. Siku hizo Yohane Mbatizaji alitokea, akaanza kuhubiri katika jangwa la Yudea:
  
2. "Tubuni, maana Ufalme wa mbinguni umekaribia."
  
3. Huyu Yohane ndiye yule ambaye nabii Isaya alinena juu yake aliposema: "Sauti ya mtu imesikika jangwani: `Mtayarishieni Bwana njia yake,nyoosheni vijia vyake."`
  
4. Yohane alivaa vazi lililoshonwa kwa manyoya ya ngamia, na ukanda wa ngozi kiunoni mwake. Chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwituni.
  
5. Basi, watu kutoka Yerusalemu, kutoka mkoa wote wa Yudea na sehemu zote za kandokando ya mto Yordani, walimwendea,
  
6. wakaziungama dhambi zao, naye akawabatiza katika mto Yordani.
  
7. Lakini alipowaona Mafarisayo wengi na Masadukayo wanamjia ili awabatize, aliwaambia, "Enyi kizazi cha nyoka! Ni nani aliyewadokezeakwamba mnaweza kuiepuka ghadhabu inayokuja?
  
8. Onyesheni basi kwa matendo, kwamba mmetubu kweli.
  
9. Msidhani kwamba mtaweza kujitetea kwa kusema, `Baba yetu ni Abrahamu!` Nawaambieni hakika, Mungu anaweza kuyafanya mawe haya yawewatoto wa Abrahamu.
  
10. Basi, shoka liko tayari kuikata mizizi ya miti; hivyo, kila mti usiozaa matunda mazuri, utakatwa na kutupwa motoni.
  
11. Mimi ninawabatizeni kwa maji kuonyesha kwamba mmetubu. Lakini yule anayekuja baada yangu ana uwezo kuliko mimi. Mimi sistahili hatakubeba viatu vyake. Yeye atawabatizeni kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.
  
12. Yeye anashika mkononi chombo cha kupuria nafaka, ili aipure nafaka yake; akusanye ngano ghalani, na makapi ayachome kwa moto usiozimika."ic
  
13. Wakati huo Yesu alitoka Galilaya akafika katika mto Yordani, akamwendea Yohane ili abatizwe naye.
  
14. Lakini Yohane alijaribu kumzuia akisema, "Je, wewe unakuja kwangu? Mimi hasa ndiye ninayehitaji kubatizwa nawe."
  
15. Lakini Yesu akamjibu, "Acha tu iwe hivyo kwa sasa, maana kwa namna hii inafaa tuyatekeleze yale yote Mungu anayotaka." Hapo Yohaneakakubali.
  
16. Mara tu Yesu alipokwisha batizwa, alitoka majini; na ghafla mbingu zikafunguka, akaona Roho wa Mungu akishuka kama njiwa na kutua juuyake.
  
17. Sauti kutoka mbinguni ikasema, "Huyu ndiye Mwanangu mpendwa, nimependezwa naye."


Search in:
Terms:

Vote and Comment on Facebook:Recommend This Page:
Post on Facebook Add to your del.icio.us Digg this story StumbleUpon Twitter Google Plus Post on Tumblr Add to Reddit Pin this story Linkedin Google Bookmark Blogger
Insert Your Personal Insight:

Please do not make mean comments and follow the biblical and spiritual character of this forum. If, however unpleasant situations arise, we request to flag it to us in order to evaluate the situation.

Text source: Swahili New Testament, public domain.

This project is based on delivering free-of-charge the Word of the Lord in all the world by using electronic means. If you want to contact us, you can do this by writing to the following e-mail: bible-study.xyz@hotmail.com


SELECT VERSION

COMPARE WITH OTHER BIBLES