Bible Study: FrontPage




 

Mathayo, Chapter 4

Bible Study - Mathayo 4 - Swahili - Swahili New Testament - Web
 
 
 
Comment!       Comment Disqus!
  
1. Kisha Roho alimwongoza Yesu mpaka jangwani ili ajaribiwe na Ibilisi.
  
2. Akafunga siku arubaini mchana na usiku, na mwishowe akaona njaa.
  
3. Basi, mshawishi akamjia, akamwambia, "Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, amuru mawe haya yawe mikate."
  
4. Yesu akamjibu, "Imeandikwa katika Maandiko Matakatifu: `Binadamu hataishi kwa mikate tu, ila kwa kila neno asemalo Mungu."`
  
5. Kisha Ibilisi akamchukua mpaka Yerusalemu, mji mtakatifu, akamweka juu ya mnara wa hekalu,
  
6. akamwambia, "Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, jitupe chini; maana imeandikwa: `Mungu atawaamuru malaika wake kwa ajili yako;watakuchukua mikononi mwao, usije ukajikwaa kwenye jiwe."`
  
7. Yesu akamwambia, "Imeandikwa pia: `Usimjaribu Bwana, Mungu wako."`
  
8. Kisha Ibilisi akamchukua mpaka juu ya mlima mrefu, akamwonyesha falme zote za ulimwengu na fahari zake,
  
9. akamwambia, "Hivi vyote nitakupa kama tu ukipiga magoti na kuniabudu."
  
10. Hapo, Yesu akamwambia, "Nenda zako Shetani! Imeandikwa: `Utamwabudu Bwana Mungu wako na kumtumikia yeye peke yake."`
  
11. Basi, Ibilisi akamwacha, na malaika wakaja, wakamhudumia.
  
12. Yesu aliposikia kwamba Yohane ametiwa gerezani alikwenda Galilaya.
  
13. Aliondoka Nazareti, akaenda Kafarnaumu, mji ulio kando ya bahari ya Genesareti, mpakani mwa wilaya za Zabuloni na Naftali, akakaa huko.
  
14. Ndivyo lilivyotimia lile neno lililosemwa kwa njia ya nabii Isaya:
  
15. "Nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali, kuelekea baharini ng`ambo ya mto Yordani, Galilaya nchi ya watu wa Mataifa!
  
16. Watu waliokaa gizani wameona mwanga mkubwa. Nao walioishi katika nchi ya giza na kivuli cha kifo, mwanga umewaangazia!"
  
17. Tangu wakati huo Yesu alianza kuhubiri akisema, "Tubuni, maana ufalme wa mbinguni umekaribia!"
  
18. Yesu alipokuwa anatembea kando ya ziwa Galilaya, aliwaona ndugu wawili wavuvi; Simoni (aitwae Petro) na Andrea, ndugu yake; walikuwawakivua samaki kwa nyavu ziwani.
  
19. Basi, akawaambia, "Nifuateni, nami nitawafanya ninyi wavuvi wa watu."
  
20. Mara wakaziacha nyavu zao, wakamfuata. ic
  
21. Alipokwenda mbele kidogo, aliwaona ndugu wengine wawili: Yakobo na Yohane, wana wa Zebedayo. Hao walikuwa ndani ya mashua pamoja na babayao Zebedayo, wakitengeneza nyavu zao. Basi Yesu akawaita,
  
22. nao mara wakaiacha mashua pamoja na baba yao, wakamfuata.
  
23. Yesu alikuwa anakwenda kila mahali wilayani Galilaya, akifundisha katika masunagogi na kuhubiri Habari Njema juu ya ufalme wa Mungu.Aliponya kila namna ya maradhi na magonjwa waliyokuwa nayo watu.
  
24. Habari zake zikaenea katika mkoa wote wa Siria. Wagonjwa wote wenye maradhi ya kila namna na wale waliosumbuliwa na kila namna ya taabu:waliopagawa na pepo, wenye kifafa na watu waliokuwa wamelemaa,walipelekwa kwake; naye akawaponya wote.
  
25. Makundi mengi ya watu kutoka Galilaya, Dekapoli, Yerusalemu, Yudea na ng`ambo ya mto Yordani, walimfuata.


Search in:
Terms:

Vote and Comment on Facebook:Recommend This Page:
Post on Facebook Add to your del.icio.us Digg this story StumbleUpon Twitter Google Plus Post on Tumblr Add to Reddit Pin this story Linkedin Google Bookmark Blogger
Insert Your Personal Insight:

Please do not make mean comments and follow the biblical and spiritual character of this forum. If, however unpleasant situations arise, we request to flag it to us in order to evaluate the situation.

Text source: Swahili New Testament, public domain.

This project is based on delivering free-of-charge the Word of the Lord in all the world by using electronic means. If you want to contact us, you can do this by writing to the following e-mail: bible-study.xyz@hotmail.com


SELECT VERSION

COMPARE WITH OTHER BIBLES