Bible Study: FrontPage




 

Ufunuo wa Yohana, Chapter 2

Bible Study - Ufunuo wa Yohana 2 - Swahili - Swahili New Testament - Web
 
 
 
Comment!       Comment Disqus!
  
1. "Kwa malaika wa kanisa la Efeso andika hivi: "Huu ndio ujumbe kutoka kwake yeye ashikaye nyota saba katika mkono wake wa kulia, na ambayehutembea katikati ya vinara saba vya taa vya dhahabu.
  
2. Najua mambo yako yote; najua bidii yako na uvumilivu wako. Najua kwamba huwezi kuwavumilia watu waovu, na kwamba umewapima walewanaojisemea kuwa mitume na kumbe sio, ukagundua kwamba ni waongo.
  
3. Wewe unayo saburi, umestahimili taabu nyingi kwa ajili ya jina langu, wala hukuvunjika moyo.
  
4. Lakini ninayo hoja moja juu yako: wewe hunipendi tena sasa kama pale awali.
  
5. Basi, pakumbuke pale ulipokuwa kabla ya kuanguka, ukayaache madhambi yako, na kufanya kama ulivyofanya pale awali. La sivyo, naja kwako nakukiondoa kinara chako mahali pake.
  
6. Lakini nakusifu juu ya kitu kimoja: wewe unayachukia wanayoyatenda Wanikolai kama ninavyoyachukia mimi.
  
7. "Aliye na masikio, basi, na asikie yale Roho anayoyaambia makanisa! "Wale wanaoshinda nitawapa haki ya kula matunda ya mti wa uzima uliokondani ya bustani ya Mungu.
  
8. "Kwa malaika wa kanisa la Smurna andika hivi: "Huu ndio ujumbe kutoka kwake yeye wa kwanza na wa mwisho, ambaye alikufa na akaishi tena.
  
9. Najua taabu zako; najua pia umaskini wako, ingawaje kwa kweli wewe ni tajiri; najua kashfa walizokufanyia wale wanaojiita Wayahudi lakini siWayahudi wa kweli, bali ni kundi lake Shetani.
  
10. Usiogope hata kidogo yale ambayo itakulazimu kuteseka. Sikiliza! Ibilisi anataka kuwajaribu kwa kuwatia baadhi yenu gerezani; nanyimtapata dhiki kwa muda wa siku kumi. Muwe waaminifu hata mpaka kufa,nami nitawapeni taji ya uzima.
  
11. "Aliye na masikio, basi, na asikie yale Roho anayoyaambia makanisa! "Wale wanaoshinda hawataumizwa na kifo cha pili.
  
12. "Kwa malaika wa kanisa la Pergamoni andika hivi: "Huu ndio ujumbe wake yeye aliye na upanga mkali wenye kuwili.
  
13. Najua unakoishi: Wewe unaishi kwenye makao makuu ya Shetani! Lakini bado unashikilia jina langu; hukuikana imani yako kwangu hata sikuzile Antipa shahidi wangu mwaminifu, alipouawa pale mahali anapoishiShetani.
  
14. Lakini ninayo machache dhidi yako: baadhi yenu ni wafuasi wa Balaamu aliyemfundisha Balaki kuwatega wana wa Israeli wale vyakulavilivyotambikiwa sanamu za kufanya uzinzi.
  
15. Vivyo hivyo, wako pia miongoni mwenu watu wanaofuata mafundisho ya Wanikolai.
  
16. Basi, achana na madhambi yako. La sivyo, nitakuja kwako upesi na kupigana na watu hao kwa upanga utokao kinywani mwangu.
  
17. "Aliye na masikio, basi, na asikie yale Roho anayoyaambia makanisa! "Wale wanaoshinda nitawapa ile mana iliyofichika. Nitawapa pia jiwejeupe lililoandikwa jina jipya ambalo hakuna mtu aliyelijua isipokuwatu wale wanaolipokea.
  
18. "Kwa malaika wa kanisa la Thuatira andika hivi: "Huu ndio ujumbe wa Mwana wa Mungu, ambaye macho yake yametameta kama moto, na miguu yakeinang`aa kama shaba iliyosuguliwa.
  
19. Najua mambo yako yote. Najua upendo wako, imani yako, utumishi wako na uvumilivu wako. Wewe unafanya vizuri zaidi sasa kuliko pale awali.
  
20. Lakini nina hoja moja juu yako: wewe unamvumilia yule mwanamke Yezabeli anayejiita nabii wa Mungu. Yeye huwafundisha na kuwapotoshawatumishi wangu wafanye uzinzi na kula vyakula vilivyotambikiwasanamu.
  
21. Nimempa muda wa kutubu dhambi zake, lakini hataki kuachana na uzinzi wake.
  
22. Sikiliza! Sasa namtupa kitandani ambapo yeye pamoja na wote waliofanya uzinzi naye watapatwa na mateso makali. Naam, nitafanyahivyo, kama wasipotubu matendo yao mabaya waliyotenda naye.
  
23. Tena nitawaua wafuasi wake, ili makanisa yote yatambue kwamba mimi ndiye ninayechunguza mioyo na fikira za watu.
  
24. "Lakini ninyi wengine mlioko huko Thuatira ambao hamfuati mafundisho yake Yezabeli, na ambao hamkujifunza kile wanachokiita `Siri yaShetani`, nawaambieni kwamba sitawapeni mzigo mwingine.
  
25. Lazima mzingatie yale mliyo nayo sasa mpaka nitakapokuja.
  
26. "Wanaoshinda, na wale watakaozingatia mpaka mwisho kutenda ninayotaka, nitawapa mamlaka juu ya mataifa. Naam, nitawapa uwezouleule nilioupokea kwa Baba: yaani, watayatawala mataifa kwa fimbo yachuma na kuyavunjavunja kama chombo cha udongo. Tena nitawapa nyota yaasubuhi.
  
27. []
  
28. []
  
29. "Aliye na masikio, basi, na ayasikie yale Roho anayoyaambia makanisa!


Search in:
Terms:

Vote and Comment on Facebook:Recommend This Page:
Post on Facebook Add to your del.icio.us Digg this story StumbleUpon Twitter Google Plus Post on Tumblr Add to Reddit Pin this story Linkedin Google Bookmark Blogger
Insert Your Personal Insight:

Please do not make mean comments and follow the biblical and spiritual character of this forum. If, however unpleasant situations arise, we request to flag it to us in order to evaluate the situation.

Text source: Swahili New Testament, public domain.

This project is based on delivering free-of-charge the Word of the Lord in all the world by using electronic means. If you want to contact us, you can do this by writing to the following e-mail: bible-study.xyz@hotmail.com


SELECT VERSION

COMPARE WITH OTHER BIBLES