Bible Study: FrontPage




 

Ufunuo wa Yohana, Chapter 3

Bible Study - Ufunuo wa Yohana 3 - Swahili - Swahili New Testament - Web
 
 
 
Comment!       Comment Disqus!
  
1. "Kwa malaika wa kanisa la Sarde andika hivi: "Huu ndio ujumbe kutoka kwake yeye aliye na roho saba za Mungu na nyota saba. Nayajua mamboyako yote; najua unajulikana kuwa na uhai kumbe umekufa!
  
2. Amka! Imarisha chochote chema kilichokubakia kabla nacho hakijatoweka kabisa. Maana, mpaka sasa, sijayaona matendo yako kuwa ni makamilifumbele ya Mungu wangu.
  
3. Kumbuka, basi, yale uliyofundishwa na jinsi ulivyoyasikia, uyatii na ubadili nia yako mbaya. Usipokesha nitakujia ghafla kama mwizi, nawala hutaijua saa nitakapokujia.
  
4. Lakini wako wachache huko Sarde ambao hawakuyachafua mavazi yao. Hao wanastahili kutembea pamoja nami wakiwa wamevaa mavazi meupe.
  
5. "Wale wanaoshinda, watavikwa mavazi meupe kama hao. Nami sitayafuta majina yao kutoka katika kitabu cha uzima; tena nitawakiri kwamba niwangu mbele ya Baba yangu na mbele ya malaika wake.
  
6. "Aliye na masikio, basi, na ayasikie yale Roho anayoyaambia makanisa!
  
7. "Kwa malaika wa kanisa la Filadelfia andika hivi: "Huu ndio ujumbe kutoka kwake yeye aliye mtakatifu na wa kweli, ambaye anao ule ufunguowa Daudi, na ambaye hufungua na hakuna mtu awezaye kufungua.
  
8. Nayajua mambo yako yote! Sasa, nimefungua mbele yako mlango ambao hakuna mtu awezaye kuufunga; najua kwamba ingawa huna nguvu sana, hatahivyo, umezishika amri zangu, umelitii neno langu wala hukulikana jinalangu.
  
9. Sikiliza! Nitawapeleka kwako watu wa kundi lake Shetani, watu ambao hujisema kuwa ni Wayahudi, kumbe ni wadanganyifu. Naam, nitawapelekakwako na kuwafanya wapige magoti mbele yako wapate kujua kwamba kwelinakupenda wewe.
  
10. Kwa kuwa wewe umezingatia agizo langu la kuwa na uvumilivu, nami pia nitakutegemeza salama wakati ule wa dhiki inayoujia ulimwengu mzimakuwajaribu wote wanaoishi duniani.
  
11. Naja kwako upesi! Linda, basi, ulicho nacho sasa, ili usije ukanyang`anywa na mtu yeyote taji yako ya ushindi.
  
12. "Wale wanaoshinda nitawafanya wawe minara katika Hekalu la Mungu wangu, na hawatatoka humo kamwe. Pia nitaandika juu yao jina la Munguwangu na jina la mji wa Mungu wangu, yaani Yerusalemu mpya, mji ambaoutashuka kutoka juu mbinguni kwa Mungu wangu. Tena nitaandika juu yaojina langu jipya.
  
13. "Aliye na masikio, basi, na ayasikie yale Roho anayoyaambia makanisa!
  
14. "Kwa malaika wa kanisa la Laodikea andika hivi: "Huu ndio ujumbe kutoka kwake yeye aitwaye `Amina`. Yeye ni shahidi mwaminifu na wakweli, ambaye ni chanzo cha viumbe vyote alivyoumba Mungu.
  
15. Nayajua mambo yako yote! Najua kwamba wewe si baridi wala si moto. Afadhali ungekuwa kimojawapo: baridi au moto.
  
16. Basi, kwa kuwa hali yako ni vuguvugu, si baridi wala si moto, nitakutapika!
  
17. Wewe unajisema, `Mimi ni tajiri; ninajitosheleza, sina haja ya kitu chochote.` Kumbe, hujui kwamba wewe ni mnyonge, unahitaji kuhurumiwa,maskini, kipofu tena uko uchi!
  
18. Nakushauri ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto upate kuwa tajiri kweli. Tena afadhali ununue pia vazi jeupe, uvae na kufunikaaibu ya uchi wako. Nunua pia mafuta ukapake machoni pako upate kuona.
  
19. Mimi ndiye mwenye kumwonya na kumrudi yeyote ninayempenda. Kwa hiyo kaza moyo, achana na dhambi zako.
  
20. Sikiliza! Mimi nasimama mlangoni na kubisha hodi. Mtu akisikia sauti yangu na kufungua mlango, nitaingia nyumbani kwake na kula chakulapamoja naye, naye atakula pamoja nami.
  
21. "Wale wanaoshinda nitawaketisha pamoja nami juu ya kiti changu cha enzi, kama vile mimi mwenyewe nilivyoshinda nikaketi pamoja na Babayangu juu ya kiti chake cha enzi.
  
22. "Aliye na masikio, basi, na ayasikie yale Roho anayoyaambia makanisa!"


Search in:
Terms:

Vote and Comment on Facebook:Recommend This Page:
Post on Facebook Add to your del.icio.us Digg this story StumbleUpon Twitter Google Plus Post on Tumblr Add to Reddit Pin this story Linkedin Google Bookmark Blogger
Insert Your Personal Insight:

Please do not make mean comments and follow the biblical and spiritual character of this forum. If, however unpleasant situations arise, we request to flag it to us in order to evaluate the situation.

Text source: Swahili New Testament, public domain.

This project is based on delivering free-of-charge the Word of the Lord in all the world by using electronic means. If you want to contact us, you can do this by writing to the following e-mail: bible-study.xyz@hotmail.com


SELECT VERSION

COMPARE WITH OTHER BIBLES