|
|
Ufunuo wa Yohana, Chapter 4
1. Baada ya hayo nilitazama nikaona mlango umefunguliwa mbinguni. Na ile sauti niliyoisikia pale awali ambayo ilikuwa kama sauti ya tarumbeta,ikasema, "Njoo hapa juu nami nitakuonyesha mambo yatakayotukiabaadaye."
2. Mara nikachukuliwa na Roho. Kumbe, huko mbinguni kuna kiti cha enzi na juu yake ameketi mmoja.
3. Huyo aliyeketi juu yake alikuwa kama almasi na jiwe zuri jekundu. Upinde wa mvua ulikuwa unang`aa kama zumaridi na ulikizunguka kiti chaenzi pande zote.
4. Kulikuwa na duara la viti ishirini na vinne kukizunguka kiti cha enzi, na juu ya viti hivyo wazee ishirini na wanne walikuwa wameketiwamevaa mavazi meupe na taji za dhahabu vichwani.
5. Umeme, sauti na ngurumo, vilikuwa vinatoka kwenye hicho kiti cha enzi. Taa saba za moto zilikuwa zinawaka mbele ya hicho kiti cha enzi.Taa hizo ni roho saba za Mungu.
6. Mbele ya kiti cha enzi kulikuwa na kitu kama bahari ya kioo, angavu kama jiwe linga`aalo sana. Katika pande zote za hicho kiti cha enzi nakukizunguka, kilikuwa na viumbe hai vinne. Viumbe hivyo vilikuwavimejaa macho mbele na nyuma.
7. Kiumbe cha kwanza kulikuwa kama simba, cha pili kama ng`ombe, cha tatu kilikuwa na sura kama mtu, na cha nne kilikuwa kama taianayeruka.
8. Viumbe hivyo vinne vilikuwa na mabawa sita kila kimoja, na vilikuwa vimejaa macho, ndani na nje. Usiku na mchana, bila kupumzika huimba:"Mtakatifu, mtakatifu, mtakatifu ni Bwana, Mungu Mwenye Uwezo,aliyekuwako, aliyeko na anayekuja!"
9. Kila mara viumbe vinne vilipoimba nyimbo za kumtukuza, kumheshimu na kumshukuru huyo aliyeketi juu ya kiti cha enzi, ambaye anaishi milelena milele,
10. wale wazee ishirini na wanne hujiangusha mbele ya huyo aliyeketi juu ya kiti cha enzi na kumwabudu huyo ambaye anaishi milele na milele; nahuziweka taji zao mbele ya kiti cha enzi wakisema:
11. "Wewe ni Bwana na Mungu wetu, unastahili utukufu na heshima na nguvu; maana wewe uliumba vitu vyote, na kwa matakwa yako kila kitukimepewa uhai na uzima."
|
|
Text source: Swahili New Testament, public domain.
|
| |
| This project is based on delivering free-of-charge the Word of the Lord in all the world by using electronic means. If you want to contact us, you can do this by writing to the following e-mail: bible-study.xyz@hotmail.com |
|
|
|
SELECT VERSION
COMPARE WITH OTHER BIBLES
|
|