Bible Study: FrontPage




 

Ayubu, Chapter 3

Bible Study - Ayubu 3 - Swahili - Swahili Union Bible - Web
 
 
 
Comment!       Comment Disqus!
  
1. Baada ya hayo Ayubu akafunua kinywa chake, na kuilaani siku yake.
  
2. Ayubu akajibu, na kusema;
  
3. Na ipotelee mbali ile siku niliyozaliwa mimi, Na ule usiku uliosema, Mtoto mume ametungishwa mimba.
  
4. Siku hiyo na iwe giza; Mungu asiiangalie toka juu, Wala mwanga usiiangazie.
  
5. Ishikwe na giza, giza tupu, kuwa yake; Wingu na likae juu yake; Chote kiifanyacho siku kuwa giza na kiitishe.
  
6. Tena usiku huo, na ushikwe na giza kuu; Usihesabiwe katika siku za mwaka; Wala kutiwa katika hesabu ya miezi.
  
7. Tazama, usiku huo na uwe tasa; Wala isiwe ndani yake sauti ya shangwe.
  
8. Na waulaani hao waulaanio mchana, Hao walio tayari kumwamsha huyo lewiathani.
  
9. Nyota za mapambazuko yake na ziwe giza; Na utafute mwanga lakini usiupate; Wala usiyaone makope ya asubuhi;
  
10. Kwa sababu haukuifunga milango ya tumbo la mamangu. Wala kunifichia taabu machoni.
  
11. Mbona si kufa mimi tokea mimbani? Mbona nisitoe roho hapo nilipotoka tumboni?
  
12. Mbona hayo magoti kunipokea? Au hayo maziwa, hata nikanyonya?
  
13. Maana hapo ningelala na kutulia; Ningelala usingizi; na kupata kupumzika;
  
14. Pamoja na wafalme na washauri wa dunia, Hao waliojijengea maganjoni;
  
15. Au pamoja na wakuu wenye dhahabu, Waliozijaza fedha nyumba zao;
  
16. Au, kama kuzikwa mimba iliyoharibika, nisingekuwako; Kama wachanga wasiouona mwanga kabisa.
  
17. Huko waovu huacha kusumbua; Huko nako hao waliochoka wapumzika
  
18. Huko wafungwa waona raha pamoja; Hawaisikii sauti yake msimamizi.
  
19. Wakuu na wadogo wako huko; Mtumishi yu huru kwa bwana wake.
  
20. Mbona yeye aliye mashakani kupewa mwanga, Na hao wenye uchungu rohoni kupewa uhai;
  
21. Ambao wangojea mauti, lakini hawayapati; Na kuyachimbulia zaidi ya kutafuta hazina iliyostirika;
  
22. Ambao wafurahi mno, Na kushangilia watakapoliona kaburi?
  
23. Kwa nini mtu aliyezibiwa njia kupewa mwanga, Ambaye Mungu amemzingira kwa ukingo?
  
24. Kwani kuugua kwangu kwaja kana kwamba ni chakula, Na kunguruma kwangu kumemiminika kama maji.
  
25. Maana jambo hilo nichalo hunipata, Nalo linitialo hofu hunijilia.
  
26. Mimi sioni raha, wala situlii, wala kupumzika; Lakini huja taabu.


Search in:
Terms:

Vote and Comment on Facebook:Recommend This Page:
Post on Facebook Add to your del.icio.us Digg this story StumbleUpon Twitter Google Plus Post on Tumblr Add to Reddit Pin this story Linkedin Google Bookmark Blogger
Insert Your Personal Insight:

Please do not make mean comments and follow the biblical and spiritual character of this forum. If, however unpleasant situations arise, we request to flag it to us in order to evaluate the situation.

Text source: This text is in the public domain, downloaded from http://www.unboundbible.org, compiled by biblephone2008@gmail.com.

This project is based on delivering free-of-charge the Word of the Lord in all the world by using electronic means. If you want to contact us, you can do this by writing to the following e-mail: bible-study.xyz@hotmail.com


SELECT VERSION

COMPARE WITH OTHER BIBLES