Bible Study: FrontPage




 

Ayubu, Chapter 4

Bible Study - Ayubu 4 - Swahili - Swahili Union Bible - Web
 
 
 
Comment!       Comment Disqus!
  
1. Ndipo huyo Elifazi, Mtemani, akajibu na kusema,
  
2. Mtu akijaribu kuzungumza nawe, je! Utaona ni vibaya? Lakini ni nani awezaye kujizuia asinene?
  
3. Tazama, wewe umewafunza watu wengi, Nawe umeitia nguvu mikono iliyokuwa minyonge.
  
4. Maneno yako yamemtegemeza huyo aliyekuwa anaanguka, Nawe umeyaimarisha magoti manyonge.
  
5. Lakini sasa haya yamekufikilia wewe, nawe wafa moyo; Yamekugusa, nawe wafadhaika.
  
6. Je! Dini yako siyo mataraja yako, Na matumaini yako si huo uelekevu wa njia zako?
  
7. Kumbuka, tafadhali, ni nani aliyeangamia akiwa hana hatia? Au hao waelekevu, walikatiliwa mbali wapi?
  
8. Kama mimi nilivyoona, hao walimao maovu, Na kupanda madhara, huvuna yayo hayo.
  
9. Kwa pumzi za Mungu huangamia. Na kwa kuvuma kwa hasira zake humalizika.
  
10. Kunguruma kwake simba, na sauti ya simba mkali, Na meno ya simba wachanga, yamevunjika.
  
11. Simba mzee huangamia kwa kukosa mawindo, Nao watoto wa simba mke wametawanyika mbalimbali.
  
12. Basi, nililetewa neno kwa siri, Sikio langu likasikia manong'ono yake.
  
13. Katika mawazo yaliyotoka katika maono ya usiku, Hapo usingizi mzito uwaangukiapo wanadamu.
  
14. Hofu iliniangukia na kutetema, Iliyoitetemesha mifupa yangu yote.
  
15. Ndipo pepo ilipita mbele ya uso wangu; Na nywele za mwili wangu zilisimama.
  
16. Hiyo pepo ilisimama kimya, nisiweze kutambua sura zake, Mfano ulikuwa mbele ya macho yangu; Kulikuwa kimya, nami nilisikia sauti, ikinena,
  
17. Je! Binadamu atakuwa na haki kuliko Mungu? Je! Mtu atakuwa safi kuliko Muumba wake?
  
18. Tazama, yeye hawategemei watumishi wake; Na malaika zake huwahesabia upuzi;
  
19. Je! Si zaidi sana hao wakaao katika nyumba za udongo, Ambazo misingi yao i katika mchanga, Hao waliosetwa mbele ya nondo!
  
20. Kati ya asubuhi na jioni huvunjwa-vunjwa; Waangamia milele wala hapana atiaye moyoni.
  
21. Je! Kamba ya hema yao haikung'olewa ndani yao? Wafa, kisha hali hawana akili.


Search in:
Terms:

Vote and Comment on Facebook:Recommend This Page:
Post on Facebook Add to your del.icio.us Digg this story StumbleUpon Twitter Google Plus Post on Tumblr Add to Reddit Pin this story Linkedin Google Bookmark Blogger
Insert Your Personal Insight:

Please do not make mean comments and follow the biblical and spiritual character of this forum. If, however unpleasant situations arise, we request to flag it to us in order to evaluate the situation.

Text source: This text is in the public domain, downloaded from http://www.unboundbible.org, compiled by biblephone2008@gmail.com.

This project is based on delivering free-of-charge the Word of the Lord in all the world by using electronic means. If you want to contact us, you can do this by writing to the following e-mail: bible-study.xyz@hotmail.com


SELECT VERSION

COMPARE WITH OTHER BIBLES