Bible Study: FrontPage




 

Mithali, Chapter 10

Bible Study - Mithali 10 - Swahili - Swahili Union Bible - Web
 
 
 
Comment!       Comment Disqus!
  
1. Mwana mwenye hekima humfurahisha babaye; Bali mwana mpumbavu ni mzigo wa mamaye.
  
2. Hazina za uovu hazifaidii kitu; Bali haki huokoa na mauti.
  
3. Bwana hataiacha nafsi ya mwenye haki ife na njaa; Bali tamaa ya mtu mwovu huisukumia mbali.
  
4. Atendaye mambo kwa mkono mlegevu huwa maskini; Bali mkono wake aliye na bidii hutajirisha.
  
5. Akusanyaye wakati wa hari ni mwana mwenye hekima; Bali asinziaye wakati wa mavuno ni mwana mwenye kuaibisha.
  
6. Baraka humkalia mwenye haki kichwani; Bali jeuri hufunika kinywa chake mtu mwovu.
  
7. Kuwakumbuka wenye haki huwa na baraka; Bali jina la mtu mwovu litaoza.
  
8. Aliye na akili moyoni mwake atapokea agizo; Bali mpumbavu mwenye maneno mengi ataanguka.
  
9. Aendaye kwa unyofu huenda salama; Bali apotoshaye njia zake atajulikana.
  
10. Akonyezaye kwa jicho huleta masikitiko; Bali mpumbavu mwenye maneno mengi ataanguka.
  
11. Kinywa chake mwenye haki ni chemchemi ya uzima; Bali jeuri hufunika kinywa chake mtu mwovu,
  
12. Kuchukiana huondokesha fitina; Bali kupendana husitiri makosa yote.
  
13. Hekima hupatikana midomoni mwa mwenye ufahamu; Bali fimbo hufaa kwa mgongo wake asiye na ufahamu.
  
14. Watu wenye akili huweka akiba ya maarifa; Bali kinywa cha mpumbavu ni uangamivu ulio karibu.
  
15. Mali ya mtu tajiri ni mji wake wa nguvu; Uangamivu wa maskini ni umaskini wao.
  
16. Kazi yake mwenye haki huuelekea uzima; Mazao ya wabaya huuelekea dhambi.
  
17. Akubaliye kurudiwa huwa katika njia ya uzima; Bali yeye aachaye maonyo hukosa.
  
18. Yeye afichaye chuki ana midomo ya uongo, Na yeye asingiziaye ni mpumbavu.
  
19. Katika wingi wa maneno hapakosi kuwa na maovu; Bali yeye azuiaye midomo yake hufanya akili.
  
20. Ulimi wa mwenye haki ni kama fedha teule; Moyo wa mtu mbaya haufai kitu.
  
21. Midomo ya mwenye haki hulisha watu wengi; Bali wapumbavu hufa kwa kuwa hawana ufahamu.
  
22. Baraka ya Bwana hutajirisha, Wala hachanganyi huzuni nayo.
  
23. Kwa mpumbavu kutenda maovu ni kama mchezo; Bali mtu mwenye ufahamu ana hekima.
  
24. Aogopacho mtu asiye haki ndicho kitakachomjilia; Na wenye haki watapewa matakwa yao.
  
25. Kisulisuli kikiisha pita asiye haki hayuko tena; Bali mwenye haki ni msingi wa milele.
  
26. Kama siki menoni, na kama moshi machoni, Ndivyo alivyo mtu mvivu kwao wamtumao.
  
27. Kumcha Bwana kwaongeza siku za mtu; Bali miaka yao wasio haki itapunguzwa.
  
28. Matumaini yao wenye haki yatakuwa furaha; Bali kutaraji kwao wasio haki kutapotea.
  
29. Njia ya Bwana ni kimbilio lake mtu mkamilifu; Bali ni uharibifu kwao watendao maovu.
  
30. Mwenye haki hataondolewa milele; Bali wasio haki hawatakaa katika nchi.
  
31. Kinywa cha mwenye haki hutoa hekima; Bali ulimi wa ukaidi utakatiliwa mbali.
  
32. Midomo ya mwenye haki huyajua yatakayokubaliwa; Bali kinywa chao wasio haki hunena ukaidi.


Search in:
Terms:

Vote and Comment on Facebook:Recommend This Page:
Post on Facebook Add to your del.icio.us Digg this story StumbleUpon Twitter Google Plus Post on Tumblr Add to Reddit Pin this story Linkedin Google Bookmark Blogger
Insert Your Personal Insight:

Please do not make mean comments and follow the biblical and spiritual character of this forum. If, however unpleasant situations arise, we request to flag it to us in order to evaluate the situation.

Text source: This text is in the public domain, downloaded from http://www.unboundbible.org, compiled by biblephone2008@gmail.com.

This project is based on delivering free-of-charge the Word of the Lord in all the world by using electronic means. If you want to contact us, you can do this by writing to the following e-mail: bible-study.xyz@hotmail.com


SELECT VERSION

COMPARE WITH OTHER BIBLES