Bible Study: FrontPage




 

Mithali, Chapter 11

Bible Study - Mithali 11 - Swahili - Swahili Union Bible - Web
 
 
 
Comment!       Comment Disqus!
  
1. Mizani ya hadaa ni chukizo kwa Bwana; Bali vipimo vilivyo sawasawa humpendeza.
  
2. Kijapo kiburi ndipo ijapo aibu; Bali hekima hukaa na wanyenyekevu.
  
3. Ukamilifu wao wenye haki utawaongoza Bali ukaidi wao wenye fitina utawaangamiza.
  
4. Mali hazifaidii kitu siku ya ghadhabu; Bali haki huokoa na mauti.
  
5. Haki yake mtu mkamilifu itamwongoza njia yake; Bali mtu mwovu ataanguka kwa uovu wake.
  
6. Haki yao wenye haki itawaokoa; Bali wafanyao fitina watanaswa kwa hila yao wenyewe.
  
7. Mtu mwovu atakapokufa, taraja lake lapotea; Na matumaini ya uovu huangamia.
  
8. Mwenye haki huokolewa katika dhiki, Na mtu mwovu ataiingia badala yake.
  
9. Asiyemcha Mungu humpoteza jirani yake kwa kinywa chake; Bali wenye haki watapona kwa maarifa.
  
10. Wenye haki wasitawipo, mji hufurahi; Waovu waangamiapo, watu hupiga kelele.
  
11. Mji hutukuzwa kwa mbaraka wa mwenye haki; Bali mji hupinduliwa kwa kinywa cha mwovu.
  
12. Asiye na akili humdharau mwenziwe; Bali mtu aliye na ufahamu hunyamaza.
  
13. Mwenye kitango akisingizia hufunua siri; Bali mwenye roho ya uaminifu husitiri mambo.
  
14. Pasipo mashauri taifa huanguka; Bali kwa wingi wa washauri huja wokovu.
  
15. Amdhaminiye mgeni hakosi ataumia; Achukiaye mambo ya dhamana yu salama.
  
16. Mwanamke wa adabu huheshimiwa daima; Na watu wakali hushika mali siku zote.
  
17. Mwenye rehema huitendea mema nafsi yake; Aliye mkali hujisumbua mwili wake.
  
18. Mtu mwovu hupata mshahara wa udanganyifu; Apandaye haki ana thawabu ya hakika.
  
19. Haki huelekea uzima; Afuataye maovu hufuata mauti yake mwenyewe.
  
20. Wenye kuhalifu moyoni ni chukizo kwa Bwana; Walio wakamilifu katika njia zao humpendeza.
  
21. Hakika, mtu mwovu hatakosa adhabu; Bali wazao wa wenye haki wataokoka.
  
22. Kama pete ya dhahabu katika pua ya nguruwe, Kadhalika mwanamke mzuri asiye na akili.
  
23. Haja ya mwenye haki ni mema tu; Bali kutaraji kwake mtu mwovu ni ghadhabu.
  
24. Kuna atawanyaye, lakini huongezewa zaidi; Kuna azuiaye isivyo haki, lakini huelekea uhitaji.
  
25. Nafsi ya mtu mkarimu itawandishwa; Anyweshaye atanyweshwa mwenyewe.
  
26. Awanyimaye watu nafaka, watu watamlaani; Auzaye nafaka, baraka itakuwa kichwani pake.
  
27. Atafutaye mema kwa bidii hutafuta fadhili; Atafutaye madhara, hayo yatamjia.
  
28. Azitegemeaye mali zake ataanguka; Mwenye haki atasitawi kama jani.
  
29. Ataabishaye nyumba yake mwenyewe ataurithi upepo; Mpumbavu atakuwa mtumwa wa mtu mwenye moyo wa akili.
  
30. Mazao ya mwenye haki ni mti wa uzima; Na mwenye hekima huvuta roho za watu.
  
31. Tazama, mwenye haki atalipwa duniani; Basi mwovu na mkosaji si mara nyingi zaidi?


Search in:
Terms:

Vote and Comment on Facebook:Recommend This Page:
Post on Facebook Add to your del.icio.us Digg this story StumbleUpon Twitter Google Plus Post on Tumblr Add to Reddit Pin this story Linkedin Google Bookmark Blogger
Insert Your Personal Insight:

Please do not make mean comments and follow the biblical and spiritual character of this forum. If, however unpleasant situations arise, we request to flag it to us in order to evaluate the situation.

Text source: This text is in the public domain, downloaded from http://www.unboundbible.org, compiled by biblephone2008@gmail.com.

This project is based on delivering free-of-charge the Word of the Lord in all the world by using electronic means. If you want to contact us, you can do this by writing to the following e-mail: bible-study.xyz@hotmail.com


SELECT VERSION

COMPARE WITH OTHER BIBLES