Bible Study: FrontPage




 

Mithali, Chapter 29

Bible Study - Mithali 29 - Swahili - Swahili Union Bible - Web
 
 
 
Comment!       Comment Disqus!
  
1. Aonywaye mara nyingi akishupaza shingo, Atavunjika ghafula, wala hapati dawa.
  
2. Wenye haki wakiwa na amri, watu hufurahi; Bali mwovu atawalapo, watu huugua.
  
3. Apendaye hekima humfurahisha babaye; Bali ashikamanaye na makahaba hutapanya mali.
  
4. Mfalme huithibitisha nchi kwa hukumu; Bali yeye apokeaye rushwa huipindua.
  
5. Mwenye kujipendekeza kwa jirani yake, Hutandika wavu ili kuitega miguu yake.
  
6. Kuna mtego katika kosa la mtu mbaya; Bali mwenye haki huimba na kufurahi.
  
7. Mwenye haki huyaangalia madai ya maskini; Bali mtu mbaya hana ufahamu hata ayajue.
  
8. Watu wenye dharau huwasha mji moto; Bali wenye hekima hugeuzia mbali ghadhabu.
  
9. Mwenye hekima akijadiliana na mpumbavu; Akikasirika au akicheka, pia hapana raha.
  
10. Wamwagao damu humchukia mtu mkamilifu; Bali wenye haki humtunza nafsi yake.
  
11. Mpumbavu hudhihirisha hasira yake yote; Bali mwenye hekima huizuia na kuituliza.
  
12. Mwenye kutawala akisikiliza uongo; Basi watumishi wake wote watakuwa waovu.
  
13. Maskini na mdhalimu hukutana pamoja; Bwana huwatia nuru macho yao wote wawili.
  
14. Mfalme awahukumuye maskini kwa uaminifu; Kiti chake cha enzi kitathibitika milele.
  
15. Fimbo na maonyo hutia hekima; Bali mwana aliyeachiliwa humwaibisha mamaye.
  
16. Waovu wakiongezeka, maasi huongezeka; Bali wenye haki watayatazama maanguko yao.
  
17. Mrudi mwanao naye atakustarehesha; Naam, atakufurahisha nafsi yako.
  
18. Pasipo maono, watu huacha kujizuia; Bali ana heri mtu yule aishikaye sheria.
  
19. Haitoshi mtumwa kuonywa kwa maneno; Maana ajapoyafahamu hataitika.
  
20. Je! Umemwona mtu mwenye kuhamaki katika maneno? Afadhali kumtumaini mpumbavu kuliko yeye.
  
21. Amtunduiaye mtumwa wake tangu utoto, Mwisho wake atakuwa ni mwanawe.
  
22. Mtu wa hasira huchochea ugomvi; Na mtu mwenye ghadhabu huasi sana.
  
23. Kiburi cha mtu kitamshusha; Bali mwenye roho ya unyenyekevu ataheshimiwa.
  
24. Mshiriki wa mwivi huichukia nafsi yake mwenyewe; Asikia maapizo, wala hana neno.
  
25. Kuwaogopa wanadamu huleta mtego; Bali amtumainiye Bwana atakuwa salama.
  
26. Watu wengi hutafuta upendeleo wa mkuu; Bali hukumu ya kila mtu hutoka kwa Bwana
  
27. Mtu aliye dhalimu ni chukizo kwa wenye haki; Na mnyofu wa mwenendo ni chukizo kwa waovu.


Search in:
Terms:

Vote and Comment on Facebook:Recommend This Page:
Post on Facebook Add to your del.icio.us Digg this story StumbleUpon Twitter Google Plus Post on Tumblr Add to Reddit Pin this story Linkedin Google Bookmark Blogger
Insert Your Personal Insight:

Please do not make mean comments and follow the biblical and spiritual character of this forum. If, however unpleasant situations arise, we request to flag it to us in order to evaluate the situation.

Text source: This text is in the public domain, downloaded from http://www.unboundbible.org, compiled by biblephone2008@gmail.com.

This project is based on delivering free-of-charge the Word of the Lord in all the world by using electronic means. If you want to contact us, you can do this by writing to the following e-mail: bible-study.xyz@hotmail.com


SELECT VERSION

COMPARE WITH OTHER BIBLES