Bible Study: FrontPage




 

Mithali, Chapter 30

Bible Study - Mithali 30 - Swahili - Swahili Union Bible - Web
 
 
 
Comment!       Comment Disqus!
  
1. Maneno ya Aguri bin Yake; mausia mtu huyu aliyomwambia Ithieli, naam, Ithieli na Ukali.
  
2. Hakika nimekuwa kama mnyama, wala si mtu; Wala sina ufahamu wa mwanadamu;
  
3. Wala sikujifunza hekima; Wala sina maarifa ya kumjua Mtakatifu.
  
4. Ni nani aliyepanda mbinguni na kushuka chini? Ni nani aliyekamata upepo kwa makonzi yake? Ni nani aliyeyafunga maji ndani ya nguo yake? Ni nani aliyefanya imara ncha zote za nchi? Jina lake ni nani? Na ni nani jina la mwanawe, kama wajua?
  
5. Kila neno la Mungu limehakikishwa; Yeye ni ngao yao wamwaminio.
  
6. Usiongeze neno katika maneno yake; Asije akakulaumu, ukaonekana u mwongo.
  
7. Mambo haya mawili nimekuomba; Usininyime [matatu] kabla sijafa.
  
8. Uniondolee ubatili na uongo; Usinipe umaskini wala utajiri; Unilishe chakula kilicho kadiri yangu.
  
9. Nisije nikashiba nikakukana, Nikasema, Bwana ni nani? Wala nisiwe maskini sana nikaiba, Na kulitaja bure jina la Mungu wangu.
  
10. Usimchongee mtumwa kwa bwana wake; Asije akakulaani, ukaonekana una hatia.
  
11. Kuna kizazi cha watu wamlaanio baba yao; Wala hawambariki mama yao.
  
12. Kuna kizazi cha watu walio safi machoni pao wenyewe; Ambao hawakuoshwa uchafu wao.
  
13. Kuna kizazi cha watu ambao macho yao yameinuka kama nini! Na kope zao zimeinuka sana.
  
14. Kuna kizazi cha watu ambao meno yao ni panga; Na vigego vyao ni kama visu. Ili kuwala maskini waondolewe katika nchi, Na wahitaji katika wanadamu.
  
15. Mruba anao binti wawili, Waliao, Nipe! Nipe! Kuna vitu vitatu visivyoshiba kamwe, Naam, vinne visivyosema, Basi!
  
16. Kuzimu; na tumbo lisilozaa; Nchi isiyoshiba maji; na moto usiosema, Basi!
  
17. Jicho la mtu amdhihakiye babaye, Na kudharau kumtii mamaye; Kunguru wa bondeni wataling'oa, Na vifaranga vya tai watalila.
  
18. Kuna mambo matatu yaliyo ya ajabu kwangu, Naam, kuna manne nisiyoyafahamu.
  
19. Mwendo wa tai katika hewa; Na mwendo wa nyoka juu ya mwamba; Mwendo wa merikebu katikati ya bahari; Na mwendo wa mtu pamoja na msichana.
  
20. Hivyo ndivyo mwendo wa mwanamke mzinifu; Hula, akapangusa kinywa chake, Akasema, Sikufanya uovu.
  
21. Kwa ajili ya mambo matatu nchi hutetemeka, Naam, kwa ajili ya manne haiwezi kuvumilia.
  
22. Mtumwa apatapo kuwa mfalme; Mpumbavu ashibapo chakula;
  
23. Mwanamke mwenye kuchukiza aolewapo; Na mjakazi aliye mrithi wa bibi yake.
  
24. Kuna viumbe vinne duniani vilivyo vidogo; Lakini vina akili nyingi sana.
  
25. Chungu ni watu wasio na nguvu; Lakini hujiwekea chakula wakati wa hari.
  
26. Wibari ni watu dhaifu; Lakini hujifanyia nyumba katika miamba.
  
27. Nzige hawana mfalme; Lakini huenda wote pamoja vikosi vikosi.
  
28. Mjusi hushika kwa mikono yake; Lakini yumo majumbani mwa wafalme.
  
29. Kuna watatu wenye mwendo wa kupendeza, Naam, wanne walio na mwendo mzuri.
  
30. Simba aliye hodari kupita wanyama wote; Wala hajiepushi na aliye yote;
  
31. Jimbi aendaye tambo; na beberu; Na mfalme ambaye haasiki.
  
32. Ikiwa umefanya kipumbavu kwa kujikuza; Au ikiwa umewaza mabaya; Basi weka mkono wako juu ya kinywa chako.
  
33. Kwa maana kupiga maziwa huleta siagi; Na kupiga pua hutokeza damu; kadhalika kuchochea hasira hutokeza ugomvi.


Search in:
Terms:

Vote and Comment on Facebook:Recommend This Page:
Post on Facebook Add to your del.icio.us Digg this story StumbleUpon Twitter Google Plus Post on Tumblr Add to Reddit Pin this story Linkedin Google Bookmark Blogger
Insert Your Personal Insight:

Please do not make mean comments and follow the biblical and spiritual character of this forum. If, however unpleasant situations arise, we request to flag it to us in order to evaluate the situation.

Text source: This text is in the public domain, downloaded from http://www.unboundbible.org, compiled by biblephone2008@gmail.com.

This project is based on delivering free-of-charge the Word of the Lord in all the world by using electronic means. If you want to contact us, you can do this by writing to the following e-mail: bible-study.xyz@hotmail.com


SELECT VERSION

COMPARE WITH OTHER BIBLES