Bible Study: FrontPage




 

Mithali, Chapter 31

Bible Study - Mithali 31 - Swahili - Swahili Union Bible - Web
 
 
 
Comment!       Comment Disqus!
  
1. Maneno ya mfalme Lemueli; mausia aliyofundishwa na mama yake.
  
2. Ni nini, mwanangu? Tena ni nini, mwana wa tumbo langu? Tena, ni nini mwana wa nadhiri zangu?
  
3. Usiwape wanawake nguvu zako; Wala moyo wako usiwape wale wawaharibuo wafalme.
  
4. Ee Lemueli, kunywa mvinyo hakuwafai wafalme, hakuwafai wafalme; Wala haifai wakuu waseme, Ki wapi kileo?
  
5. Wasije wakanywa na kuisahau sheria, Na kuipotosha hukumu ya mtu aliye taabuni.
  
6. Mpe kileo yeye aliye karibu na kupotea; Kampe divai yeye aliye na uchungu nafsini.
  
7. Anywe akausahau umaskini wake; Asiikumbuke tena taabu yake.
  
8. Fumbua kinywa chako kwa ajili yake aliye bubu; Uwatetee watu wote walioachwa peke yao;
  
9. Fumbua kinywa chako, uhukumu kwa haki; Uwapatie maskini na wahitaji haki yao.
  
10. Mke mwema, ni nani awezaye kumwona? Maana kima chake chapita kima cha marijani.
  
11. Moyo wa mumewe humwamini, Wala hatakosa kupata mapato.
  
12. Humtendea mema wala si mabaya, Siku zote za maisha yake.
  
13. Hutafuta sufu na kitani; Hufanya kazi yake ya mikono kwa moyo.
  
14. Afanana na merikebu za biashara; Huleta chakula chake kutoka mbali.
  
15. Tena huamka, kabla haujaisha usiku; Huwapa watu wa nyumbani mwake chakula; Na wajakazi wake sehemu zao.
  
16. Huangalia shamba, akalinunua; Kwa mapato ya mikono yake hupanda mizabibu.
  
17. Hujifunga nguvu viunoni kama mshipi; Hutia mikono yake nguvu.
  
18. Huona kama bidhaa yake ina faida; Taa yake haizimiki usiku.
  
19. Hutia mikono yake katika kusokota; Na mikono yake huishika pia.
  
20. Huwakunjulia maskini mikono yake; Naam, huwanyoshea wahitaji mikono yake.
  
21. Hawahofii theluji watu wa nyumbani mwake; Maana wote wa nyumbani mwake huvikwa nguo nyekundu.
  
22. Hujifanyia mazulia ya urembo; Mavazi yake ni kitani safi na urujuani.
  
23. Mume wake hujulikana malangoni; Aketipo pamoja na wazee wa nchi.
  
24. Hufanya nguo za kitani na kuziuza; Huwapa wafanya biashara mishipi.
  
25. Nguvu na hadhi ndiyo mavazi yake; Anaucheka wakati ujao.
  
26. Hufumbua kinywa chake kwa hekima, Na sheria ya wema i katika ulimi wake.
  
27. Huangalia sana njia za watu wa nyumbani mwake; Wala hali chakula cha uvivu.
  
28. Wanawe huondoka na kumwita heri; Mumewe naye humsifu, na kusema,
  
29. Binti za watu wengi wamefanya mema, Lakini wewe umewapita wote.
  
30. Upendeleo hudanganya, na uzuri ni ubatili; Bali mwanamke amchaye Bwana, ndiye atakayesifiwa.
  
31. Mpe mapato ya mikono yake, Na matendo yake yamsifu malangoni.


Search in:
Terms:

Vote and Comment on Facebook:Recommend This Page:
Post on Facebook Add to your del.icio.us Digg this story StumbleUpon Twitter Google Plus Post on Tumblr Add to Reddit Pin this story Linkedin Google Bookmark Blogger
Insert Your Personal Insight:

Please do not make mean comments and follow the biblical and spiritual character of this forum. If, however unpleasant situations arise, we request to flag it to us in order to evaluate the situation.

Text source: This text is in the public domain, downloaded from http://www.unboundbible.org, compiled by biblephone2008@gmail.com.

This project is based on delivering free-of-charge the Word of the Lord in all the world by using electronic means. If you want to contact us, you can do this by writing to the following e-mail: bible-study.xyz@hotmail.com


SELECT VERSION

COMPARE WITH OTHER BIBLES