|
|
Zaburi, Chapter 113
1. Haleluya. Enyi watumishi wa Bwana, sifuni, Lisifuni jina la Bwana.
2. Jina la Bwana lihimidiwe Tangu leo na hata milele.
3. Toka maawio ya jua hata machweo yake Jina la Bwana husifiwa.
4. Bwana ni mkuu juu ya mataifa yote, Na utukufu wake ni juu ya mbingu.
5. Ni nani aliye mfano wa Bwana, Mungu wetu aketiye juu;
6. Anyenyekeaye kutazama, Mbinguni na duniani?
7. Humwinua mnyonge kutoka mavumbini, Na kumpandisha maskini kutoka jaani.
8. Amketishe pamoja na wakuu, Pamoja na wakuu wa watu wake.
9. Huweka nyumbani mwanamke aliye tasa, Awe mama ya watoto mwenye furaha.
|
|
Text source: This text is in the public domain, downloaded from http://www.unboundbible.org, compiled by biblephone2008@gmail.com.
|
| |
| This project is based on delivering free-of-charge the Word of the Lord in all the world by using electronic means. If you want to contact us, you can do this by writing to the following e-mail: bible-study.xyz@hotmail.com |
|
|
|
SELECT VERSION
COMPARE WITH OTHER BIBLES
|
|