|
|
Zaburi, Chapter 112
1. Haleluya. Heri mtu yule amchaye Bwana, Apendezwaye sana na maagizo yake.
2. Wazao wake watakuwa hodari duniani; Kizazi cha wenye adili kitabarikiwa.
3. Nyumbani mwake mna utajiri na mali, Na haki yake yakaa milele.
4. Nuru huwazukia wenye adili gizani; Ana fadhili na huruma na haki.
5. Heri atendaye fadhili na kukopesha; Atengenezaye mambo yake kwa haki.
6. Kwa maana hataondoshwa kamwe; Mwenye haki atakumbukwa milele.
7. Hataogopa habari mbaya; Moyo wake u imara ukimtumaini Bwana.
8. Moyo wake umethibitika hataogopa, Hata awaone watesi wake wameshindwa.
9. Amekirimu, na kuwapa maskini, Haki yake yakaa milele, Pembe yake itatukuzwa kwa utukufu.
10. Asiye haki ataona na kusikitika, Atasaga meno yake na kuyeyuka, Tamaa ya wasio haki itapotea.
|
|
Text source: This text is in the public domain, downloaded from http://www.unboundbible.org, compiled by biblephone2008@gmail.com.
|
| |
| This project is based on delivering free-of-charge the Word of the Lord in all the world by using electronic means. If you want to contact us, you can do this by writing to the following e-mail: bible-study.xyz@hotmail.com |
|
|
|
SELECT VERSION
COMPARE WITH OTHER BIBLES
|
|